#SheriaYaLeo (357/366); Ujinga wa kiwango cha juu.
Binadamu tunazaliwa, kuishi na kufa.
Hivyo ndivyo maisha yamekuwepo tangu enzi na enzi na ndiyo imewezesha dunia kuendelea kuwepo.
Viumbe wanaokufa wanatoa nafasi kwa wengine wanaozaliwa.
Baadhi ya watu wanatafuta teknolojia ya kurefusha maisha au kuondoa kabisa kifo.
Huu ni ujinga wa hali ya juu, ambao pia unaambatana na ubinafsi.
Kutaka kuishi milele ni ubinafsi wa kujiangalia sisi wenyewe na kutokujali kuhusu wengine ambao bado hata hawajazaliwa.
Na pia pata picha ya dunia ambayo watu hawafi, ni idadi kiasi gani ya watu wanaweza kuenea kwenye hii dunia kama kufakuwa hakuna kifo kabisa?
Kifo kina manufaa mengi kwetu binafsi na kwa dunia kwa ujumla. Kujua kuna kifo kunatupa msukumo wa kutumia muda wetu vizuri.
Na pale tunapokufa, tunatoa nafasi kwa wengine nao kuishi.
Sheria ya leo; Kukataa kifo na kupambana nacho ni ujinga wa kiwango cha juu na matusi kwa asili ya binadamu. Kudhani unaweza kuizidi asili ni kujidanganya. Asili inajiendesha kwa mpango wake ambao huwezi kuuvuruga bila madhara.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji