2854; Ng’ang’ana mpaka ufanikiwe.
Wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote huanza sawa.
Huwa wanaanza na ndoto kubwa walizonazo.
Kisha wanachukua hatua kwenye ndoto hizo.
Katika kuchukua huko hatua huwa wanakutana na changamoto na vikwazo mbalimbali.
Na hapa ndipo wanaofanikiwa na wanaoshindwa wanapotofautiana.
Wanaoshindwa huwa wanakata tamaa haraka pale wanapokutana na vikwazo na changamoto mbalimbali.
Wanaona mambo ni magumu na hayawezekani, hivyo wanaachana nayo na kwenda kujaribu mambo mengine.
Wanaofanikiwa huwa hawakati tamaa hata kama wamekutana na changamoto na vikwazo gani.
Wao huwa wanaendelea kufanya bila kuacha.
Huwa wanang’ang’ana mpaka wafanikiwe.
Huo ndiyo msingi muhimu sana wa kujijengea.
Ukishachagua ni nini hasa unachotaka kwenye maisha yako, ng’ang’ana nacho mpaka ukipate.
Haijalishi umekutana na nini, endelea kufanya.
Iwe jua au mvua, wewe fanya.
Ni kupitia ung’ang’anizi ndiyo utaweza kupata chochote kile unachokitaka.
Dunia huwa ina tabia ya kuwajaribu watu kama wanataka kweli kile wanachosema wanataka.
Inawapa vikwazo na changamoto mbalimbali.
Wanaokata tamaa wanakosa, wanaong’ang’ana wanapata wanachotaka.
Hatua ya kuchukua leo;
Andika yale unayotaka kupata au kufikia. Kisha jiambie utang’ang’ana mpaka upate au kufikia. Jiambie hakuna chochote kitakachokukatisha tamaa au kukufanya uishie njiani. Utaendelea kufanya mpaka upate kile unachokitaka.
Tafakari;
Ili kufanikiwa, amua kwamba utapata unachotaka au utakufa ukiwa unakipambania. Usikubali kingine tofauti na hivyo. Msamiati wa kushindwa au kukata tamaa ufute kabisa kwenye fikra zako. Wewe unakaa kwenye mchakato bila kutoroka au kuishia njiani.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed