#SheriaYaLeo (361/366); Tumia vizuri ubongo wa dunia.

Ubongo ni kiungo chenye nguvu kubwa kwenye miili yetu. Kina nguvu ya kutuwezesha kupata chochote tunachotaka.
Kile ambacho tunakifikiri kwa muda mrefu ndiyo kinakuwa uhalisia wetu, kwa sababu ubongo unatuletea taarifa za aina hiyo zaidi.
Pamoja na nguvu hiyo kubwa ya ubongo, bado wengi wanatumia ubongo huo kwa mambo yasiyo na tija na hivyo kushindwa kufanya makubwa.

Kwa kutumia mfano huo wa ubongo, kwenye zama tunazoishi, dunia yetu ina ubongo wake ambao pia una nguvu kubwa.
Ubongo wa dunia ni mtandao wa intaneti.
Mtandao huu una taarifa nyingi sana, hivyo mtu anaweza kupata chochote anachotaka.
Mtandao wa intaneti una kila aina ya taarifa na maarifa ambayo mtu anahitaji ili kufanya makubwa.

Lakini kwa bahati mbaya sana, watu wamekuwa wanatumia mtandao huo wa intaneti kwa mambo yasiyokuwa na tija.
Wanapoteza muda kuzurura kwenye mitandao ya kijamii kitu ambacho hakiwapi manufaa yoyote.

Wewe tumia vizuri ubongo huu wa dunia, kupata maarifa na taarifa na kuzitumia kufanya makubwa.
Chochote unachotaka unaweza kukipata kwa kutumia vizuri mtandao wa intaneti.

Sheria ya leo; Badala ya kutumia mtandao wa intaneti kujifurahisha na kupoteza muda, utumie kupata maarifa na taarifa utakazotumia kufanya makubwa.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji