2858; Icheke dunia.
Katika viumbe wote waliopo hapa duniani, sisi binadamu pekee ndiyo wenye uwezo wa kucheka.
Viumbe wote wana uwezo wa kulia, hasa pale wanapokuwa na maumivu mbalimbali.
Lakini inapokuja kwenye kucheka, ni sisi binadamu pekee tunaoweza kufanya hivyo.
Tumia uwezo huo wa kucheka kuweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Icheke dunia kwa yote yanayoendelea.
Kucheka ni kiashiria cha furaha na kukubali kitu.
Lakini pia ni kiashiria cha kwamba kitu siyo kigumu kama wengi wanavyochukulia.
Kwa kuicheka dunia, maana yake umeikubali na una furaha.
Lakini pia unamaanisha hakuna chochote kigumu na cha kukutisha kwenye hii dunia.
Hilo linakupa nguvu ya kuendelea kupambana na kuikabili dunia ili kuweza kupata chochote unachotaka.
Hatua ya kuchukua leo;
Usiyape mambo uzito mkubwa kuliko yanavyostahili. Icheke dunia kwa kuona jinsi mengi yasivyo muhimu au magumu kama unavyodhani.
Pokea na kabiliana na lolote linalokujia ili uweze kufanya makubwa zaidi.
Tafakari;
Kucheka kuna nguvu kuliko kununa. Kucheka kunafungua sura na moyo wako kwa wengine, ambao wanakuwa tayari kushirikiana na wewe kwenye mambo yako mbalimbali. Cheka kwa wingi na mambo yatakuwa rahisi kuliko unavyotachukulia.
#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed