#SheriaYaLeo (362/366); Penda asili.
Kuna mambo mengi kwenye maisha yetu ambayo hayapo ndani ya udhibiti wetu.
Tunakutana na maumivu, magonjwa, kutengana na hata kifo.
Tunakutana na magumu, changamoto na hata kushindwa kwenye mambo mangi ambayo tunapanga kufanya.
Tunaweza kufanya kila kitu kwa usahihi kabisa lakini bado tukakutana na hali hizo.
Hivyo badala ya kuumia na kujiuliza kwa nini itokee kwetu, tunapaswa kukubaliana na asili na kupenda yale ambayo asili imeleta kwetu.
Tunapaswa kuyakubali na kuyatumia vyema ili kuweza kupata kile ambacho tunataka.
Maana kukataa kile ambacho tayari kimeshatokea haina manufaa yoyote, maana kimeshatokea, hakiwezi kurudi.
Ila unapokubali na kutumia vizuri chochote kilichotokea, hata kama kinaonekana kibaya, utaweza kufanya makubwa zaidi.
Sheria ya leo; Chukulia kila tukio kama mpango wa asili na jua imetokea kwa sababu. Ni wajibu wako kujifunza na kutumia vyema kila kinachotokea ili uweze kupiga hatua zaidi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji