2859; Zidisha thamani yako.

Zamani watu walikuwa wanalipwa kulingana na muda wanaofanya kazi, hivyo wengi walitengeneza mazingira ya kuonekana wanafanya kazi muda mrefu hata kama haina tija.

Siku hizi watu wanalipwa kulingana na thamani wanayoizalisha.
Hivyo kama unataka ukipwe zaidi, toa thamani zaidi.

Ukizidisha thamani unayoitoa mara 10, utaweza kuongeza kipato chako zaidi ya mara 10.

Uzuri ni kwamba, kuzidisha thamani yako ni kitu ambacho kipo ndani ya uwezo wako, kitu unachoweza kukifanya bila ya kumtegemea mtu mwingine.

Hivyo unapaswa kuanza mara moja kutoa thamani zaidi kwa chochote unachofanya.
Wape watu thamani kubwa kuliko walivyozoea na pale utakapotaka wakulipe zaidi, watakuwa tayari kufanya hivyo.

Haijalishi tayari unatoa thamani gani, bado una fursa za kutoa thamani kubwa zaidi ya unavyotoa sasa.

Hatua ya kuchukua leo;
Kwa kila unachofanya, jiulize unawezaje kutoa thamani kubwa zaidi ya unavyotoa sasa, kisha kazana kutoa thamani hiyo. Kila wakati jisukume kutoa thamani kubwa kuliko ilivyozoeleka na utaweza kutengeneza kipato kikubwa zaidi.

Tafakari;
Unalipwa kulingana na thamani unayoipeleka sokoni. Hivyo kama huridhiki na malipo unayopata sasa, njia ni moja, zidisha thamani yako zaidi.

#LetsBuildBusinesses
#NothingElseMatters
#BillionairesInTraining
#WeAllGonnaMakeIt
#WorkHardAndYouWillSucceed