#SheriaYaLeo (363/366); Anga na nyota.

Kwenye usiku usio na mawingu, liangalie anga na utaziona nyota nzuri ambazo zinalipendezesha anga.

Ukiangalia anga wakati wa mchana utaliona jua ambalo ni nyota iliyo karibu zaidi na dunia na ambayo mwanga wake unaipa uhai dunia.

Bila ya mwanga wa jua, kusingeweza kuwa na maisha hapa duniani.
Chukulia jinsi ambavyo uwepo wa jua una umuhimu kwenye maisha yote ya dunia.

Kuna teknolojia nyingi mpya ambazo zimekuja, lakini uwepo wa jua ni wa miaka na miaka na watu wamekuwa wanalitumia tangu enzi na enzi.

Kwa kuangalia anga na nyota, unajifunza mengi na kuuona ukuu wa ulimwengu mzima ambao sisi ni sehemu yake.

Sheria ya leo; Angalia anga na nyota kama vile ndiyo unaviona kwa mara ya kwanza. Kuna mengi utakayojifunza kuhusu ukuu wa ulimwengu.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji