#SheriaYaLeo (365/366); Kubali udogo wako.

Tulipokuwa watoto tulijua udogo wetu na kukubali kuna mengi ambayo yapo nje ya uwezo wetu.

Sasa tumekuwa watu wazima na kusahau udogo huo, kwa kudhani kila kitu kinapaswa kuwa ndani ya uwezo wetu.

Lakini ukiuangalia ukubwa wa ulimwengu, sisi bado ni wadogo sana.
Ukiangalia umri ambao ulimwengu umekuwepo, muda wetu ni kama tone tu kwenye bahari.

Lakini bado tunapata nguvu ya kujitutumua na mambo ambayo yapo nje kabisa ya uwezo wetu.

Tunapaswa kujikumbusha udogo wetu ukilinganisha na ukubwa na ukuu wa dunia.
Tunaweza kufanya hivyo kwa kurudi nyuma na kukumbuka kipindi tukiwa watoto. Tunarudi mpaka tukiwa mimba na hata tulipokuwa mbegu tu.
Kwa kuangalia hivyo, tunaona wazi ni kwa jinsi gani ni wadogo ukilinganisha na ulimwengu.

Nia ya zoezi hili siyo ujidharau kwamba huwezi lolote, bali kukupa unyenyekevu wa kuyakabili maisha yako kwa namna sahihi.
Kujua nini kipo ndani ya uwezo wako na nini kipo nje ya uwezo wako kisha kuchukua hatua sahihi.

Sheria ya leo; Kujua na kukubali udogo wako kunakufanya uwe mkuu na muhimu. Huo ni uwezo ambao hakuna viumbe wengine wanao na hata kwa binadamu siyo wote wanapata utambuzi wa aina hii. Utambuzi huu unakupa nguvu ya kuweza kufanya makubwa sana.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji