2869; Kifo kiko pale pale.
Kwako rafiki yangu unayeona maisha ni mafupi hivyo haina haja ya kujihangaisha.
Iwe utafanya mambo madogo au makubwa kwenye maisha yako, bado kifo kipo pale pale.
Uwe na malengo makubwa au madogo, mwisho wa hii safari yako ni kifo.
Kama hivyo ndivyo ilivyo, kwa nini usijitoe na kujisukuma ili kufanya makubwa yatakayoacha alama hapa duniani?
Kwa nini usiyatumie vyema haya maisha mafupi uliyonayo kuigusa dunia kwa namna ya kipekee kitu kitakachofanya uendelee kukumbukwa hata baada ya kufa?
Usikubali kupita hapa duniani kimya kimya kama mnyoo.
Fanya uwepo wako uwe wa kukumbukwa, kupitia yale unayofanya na alama unayoacha.
Jisukume kweli kweli utumie uwezo wako wote ulio ndani yako ili usije ukaondoka nao pale unapokufa.
Usitumie ufupi wa maisha yako kukata tamaa, badala yake utumie kufanya makubwa na kuacha alama.
Malengo yoyote uliyonayo sasa, yazidishe mara 10 na uyapambanie malengo hayo makubwa zaidi.
Ishi maish yenye maana na yanayoacha alama. Tumia kila kilicho ndani yako kabla safari hii fupi haijafika ukingoni.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe