2872; Tuongelee hili swala la uvivu.
Kwako rafiki yangu unayedhani unaweka juhudi kubwa kwenye kazi, lakini hakuna matokeo mazuri unayoyapata.
Watu wengi wamekuwa wakichanganya kushughulika na kuzalisha.
Huwa wanadhani kwa kushughulika ndiyo wanajituma hasa.
Lakini unapoyaangalia matokeo wanayozalisha, unaona kabisa kwamba hayaendani na kile wanachodai.
Mtu anakuwa yupo bize kweli kweli, lakini hakuna matokeo anayokuwa anayazalisha.
Ingekuwa kuwa bize ndiyo kufanikiwa, kila mtu tayari angekuwa na mafanikio makubwa.
Lakini mafanikio hayatokani na ubize, bali uzalishaji.
Pale unapofanya mambo yenye tija na ukayafanya kwa usahihi ndiyo unapata matokeo ambayo yanakupeleka ngazi za juu zaidi.
Hivyo basi, uvivu siyo tu kutokufanya vitu, bali hata kufanya yasiyo na tija ni uvivu.
Kuwa bize wakati huzalishi ni uvivu mkubwa.
Na watu wengi wamekuwa wanatumia hali ya ubize kuficha uvivu wao.
Kwa mfano, unajua kabisa kwamba ili biashara yako ifanikiwe, lazima uuze zaidi.
Na ili uuze zaidi unahitaji kuongea na wateja wengi zaidi.
Lakini inapofika kuongea na wateja, unakimbilia kufanya majukumu mengine ambayo hayana mchango wowote kwenye lengo la kuongeza mauzo.
Huo ndiyo uvivu ninaouongelea, unaonekana uko bize kweli, lakini kwa mambo yasiyo sahihi.
Tukubaliane kwamba uvivu siyo kutokufanya, bali hata kufanya vitu visivyo na mchango kwenye malengo yako ni uvivu.
Sasa hebu pata picha mtu ambaye hana hata malengo kabisa!
Unajionea mwenyewe kwa nini wengi hawafanikiwi kwenye maisha.
Kwa sababu ni wavivu waliojificha nyuma ya ushughulikaji ambao hauna uzalishaji.
Hatutaangalia unashughulika na kuchoka kiasi gani.
Kama unachohangaika nacho hakikupeleki kwenye malengo uliyonayo, huo ni uvivu, achana nao mara moja.
Uvivu ni dhambi kubwa sana kwenye safari ya mafanikio. Usipoiacha, kamwe hutaonja utamu wa mafanikio.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe