2877; Kusema na kufanya.

Kwako rafiki yangu ambaye huwa unawaamini watu haraka kwa maneno yao.

Unapaswa ukumbuke kwamba maneno siyo vitendo.
Kusema ni rahisi, kufanya ni ngumu.
Hivyo wengi wameishia kuwa wasemaji wenye ahadi nyingi, lakini zisizotekelezwa.

Kupunguza upotevu wa muda wako wa thamani kwa kujihusisha na watu wasio sahihi, usiwe mtu wa kukimbilia kuwaamini watu kwa maneno yao.
Badala yake angalia ushahidi wa mambo ambayo tayari wameshafanya.

Kwa zama tunazoishi sasa, ni zoezi gumu sana kuwapata wafanyaji hasa. Hilo linahitaji utulivu na uvumilivu katika kulifanyia kazi.

Watu wanaweza kuongea vizuri sana na kwa ushawishi.
Lakini kama hawana ushahidi , kuwa na tahadhari.

Kama ingekuwa maneno pekee yana nguvu ya kuleta mabadiliko, kila mtu angekuwa amepiga hatua kubwa.

Ni vile kuchukua hatua kunahitaji mtu ajitoe kweli na kumejaa vikwazo na changamoto mbalimbali.

Wewe kuwa mtu wa aina hiyo, usiwe tu mtu wa maneno mengi yasiyo na ushahidi.
Bali kuwa mtu wa vitendo, mtu wa kuchukua hatua na kuyaonyesha mafanikio.

Kwa kuzingatia hilo, utaziona fursa nyingi za kukuwezesha kupata kila unachotaka.

#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe