2883; Nadra, Mara kwa mara, Kawaida.
Kwako rafiki yangu mpendwa unayeshangazwa na jinsi mambo yanavyobadilika kwenye masha yako.
Mambo huwa yanaanza yakiwa nadra, baadaye yanakuwa mara kwa mara na hatimaye kawaida.
Nadra ni pale ambapo mambo yanakuwa hayatokei kabisa.
Yanapoanza kutokea mara chache, inashangaza mwanzoni, lakini yakiendelea kutokea yanazoeleka.
Kadiri yanavyoendelea kutokea, yanazoeleka kabisa na kuwa kitu cha kawaida ambazo kinategemewa.
Unaweza kutumia hili kwa njia mbili.
Njia ya kwanza ni kwa mambo mazuri unayotaka yatokee.
Huwa ni vigumu mwanzoni, lakini yanapoendelea kufanyika yanazoeleka.
Hivyo kama kuna kitu kizuri ambacho unataka kiwe mazoea kwenye maisha yako, wewe kifanye mara kwa mara bila kuchoka wala kukata tamaa.
Njia ya pili ni mambo mabaya ambayo hutaki yatokee.
Kwa haya, hakikisha hurusu yakatokea hata mara chache.
Yaani yazuie yasitokee kabisa.
Kwa sababu yakishaanza kutokea, yanazoeleka na baadaye kuwa sugu.
Kwa kitu chochote kibaya ambacho hutaki kiwe mazoea kwenye maisha yako, kizuie kisitokee hata mara moja.
Kama kuna tabia au vitu usivyopendezwa navyo ambavyo vinaendelea kwenye maisha yako, jua ni wewe mwenyewe umeviruhusu.
Kadhalika kwa tabia au vitu unavyopendezwa navyo lakini huvipati, kinachokosekana ni msimamo.
Kwa bahati mbaya sana huwa tunakuwa na msimamo kwenye mambo ya kijinga na kukosa msimamo kwenye mambo ya maana.
Kufanikiwa, lazima ugeuze hilo, jenga msimamo kwenye mambo ya maana na uvunje kwenye mambo yasiyo ya maana.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe