2891; Chipsi Mayai.
Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye unashangazwa na mvurugano unaojitokeza wakati wa mabadiliko.
Mabadiliko yoyote yale huwa yanaambatana na hali ya mvurugano.
Hakuna mabadiliko yenye utulivu.
Mabadiliko ni sawa na kuandaa chipsi mayai, lazima uyavunje mayai.
Kuyavunja mayai inaweza kuonekana kama ni kutaharibu, lakini chipsi zinapokuwa tayari, hilo halionekani kuwa ni uharibifu.
Kwenye kila mabadiliko, kuna mengi yatakayovunjwa kitu kitakacholeta mvurugano na kuona kama unapoteza.
Lakini hilo halipaswi kuleta hofu, badala yake unapaswa kuwa na matumaini kwamba mambo mazuri yatatokea hapo mbeleni.
Kama upo kwenye kipindi cha ukuaji wa kibiashara, mvurugano lazima utakuwepo.
Hakuna anayependa mvurugano, lakini wale wanaofanikiwa huwa wanaudhibiti vizuri.
Wasiofanikiwa wanakimbia mvurugano na hilo linakuwa kikwazo kikubwa kwao.
Usitumie hali ya mvurugano inayojitokeza kuyakataa mabadiliko. Badala yake itegemee na idhibiti vizuri.
Mabadiliko siyo rahisi ndiyo maana wengi huwa hawayafanyi. Huwa wanakuwa hawataki kujisumbua na mvurugano unaozalishwa.
Wewe ni wa tofauti, hutafuti urahisi bali unatafuta usahihi.
Simama kwenye hilo na utaweza kufanya makubwa sana.
Peleka hilo kwa timu yako pia.
Waeleze wazi kwamba kipindi cha mabadiliko kitaambatana na mvurugano.
Wasitafute njia ya kukwepa huo mvurugano, badala yake waukabili na waweze kuutumia kupiga hatua kubwa za mabadiliko zinazohitajika.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe