2894; Uko bize kufanya nini?
Kwako rafiki yangu mpendwa ambaye kila wakati uko bize kiasi cha kukosa muda wa kuyafanyia kazi yake mapya unayojifunza.
Pamoja na kuwa kwako bize, hakuna matokeo makubwa na ya tofauti unayozalisha.
Na hapo ndipo swali langu linapokuja, uko bize kufanya nini?
Kama mambo yanayokuweka bize ni yenye tija, matokeo unayopata yatakuwa na viashiria hivyo.
Kama mambo yanayokuweka nize hayana tija, utaendelea kuwa na malalamiko mengi.
Ni kawaida yetu binadamu kuwa na hali ya ujuaji, kuona kile tunachofanya tunakijua kwa kina na hivyo kujifunza vitu vipya kwenye hilo haina maana.
Hili ndiyo limekuwa kikwazo kwa wengi kujifunza na kuchukua hatua ili kupata matokeo bora.
Kuhakikisha hili la ubize haliwi kimwazo kwako, fanya zoezi hili muhimu;
Anza kwa kuandika lengo lako kubwa unalotaka kufikia. Andika kwa usahihi kabisa kile kikubwa unachotaka kukifikia.
Kisha orodhesha mambo matatu unayopaswa kuyafanya ili kufikia malengo uliyonayo.
Ni mambo gani matatu ambayo yakifanyika lazima malengo yafikiwe? Hapo ndipo muhimu kuzingatia.
Mwisho, kwenye orodha ya mambo matatu ya kufanyika, pata vitu vitatu ambavyo utavifanyia kazi kila siku bila kuacha.
Hivi ni vitu vitatu ambavyo ukivifanya kila siku bila kuacha, utazalisha matokeo makubwa na mazuri.
Hakikisha kila siku unayoianza unajua mambo matatu ya muhimu kwako kufanya ili kuyafikia malengo makubwa uliyonayo.
Hii ndiyo njia sahihi ya kuwa bize, njia yenye tija.
Tatizo la kuwa bize ni kwamba ubize huwa hauchagui nini kinafanyika.
Hata ukiianza siku yako bila mpango wowote, ghafla utajikuta tayari uko bize kwa mambo yasiyokuwa na tija yoyote kwako.
Kuamua kuwa bize kwa makusudi, kwa yale yenye tija, itakupa uwanja mpana wa kufika kule unakotaka kufika.
Kwenye haya maisha, unaweza kuchagua kuwa bize na mambo yako au dunia ikakuweka bize na mambo ya wengine.
Maisha ni yako na uchaguzi pia ni wako.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe