2930; Kokotoa thamani ya muda wako.
Rafiki yangu mpendwa,
Kupitia kurasa hizi nilikushirikisha dhana ya kuwa na thamani ya muda wako ili uweze kuutumia vyema.
Dhana hiyo ilihusisha kuupa muda thamani ya kifedha ili kutokuupoteza kwa mambo yasiyo na tija.
Wengi hawakuelewa jinsi ya kuweza kukokotoa thamani ya muda wao.
Leo unakwenda kujifunza jinsi ya kufanya hivyo.
Ukokotoaji huu wa thamani ya muda unahusisha hesabu, kitu ambacho kinaweza kisiwe pendwa kwa wengi.
Hivyo kama hizo hesabu zitakuchanganya, wewe chukulia thamani ya saa moja kuwa Tsh laki moja.
Hiyo ni namba nzuri ya kuanzia ambayo itakusukuma sana kwa yale unayofanya.
Sasa kwa wale ambao wangependa kujua hesabu za kukokotoa thamani ya muda kwa uhakika.
Kwanza unaanza na kipato ambacho unapanga kuingiza kwa mwaka, kisha unagawa kwa mwezi kisha wiki na hatimaye siku.
Kwa upande wetu litakuwa ni lengo la mauzo.
Ukishajua kiwango hicho kwa siku, kigawe kwa masaa ya kazi kwa siku.
Japokuwa tunapanga muda wa kazi kuwa masaa 16 kwa siku, siyo yote utaweza kuyatumia kwa mambo yanayozalisha tu. Kuna mambo mengine utalazimika kufanya ambayo hayawezi kuchangia kipato moja kwa moja.
Hivyo katika masaa 16 ya kazi kwa siku, chukulia 10 ambayo ndiyo unayaweka kwenye majukumu yanayochangia kwenye fedha moja kwa moja.
Hivyo lengo lako la kipato kwa siku gawa kwa masaa 10 na hapo utapata thamani ya saa yako moja.
Kwa mfano kama kwa kugawa lengo lako umepata milioni 1 kwa siku kama ndiyo lengo la mauzo, basi thamani ya saa yako moja ni milioni 1 gawa kwa 10 ambapo inakuwa ni lako moja.
Sasa basi, japo umegawa thamani ya muda kwenye masaa 10 ya siku, bado hiyo ndiyo utakayoitumia kwa masaa yote 16 ya siku.
Hivyo kwa kila unachofanya kwenye masaa hayo 16 jiulize kinamchango gani katika kuingiza tsh laki 1?
Kama kitu hakina thamani hiyo basi hukifanyi. Kama unachotaka kufanya hakiingizi fedha au kukuandaa kuingiza kiasi hicho cha fedha, unapaswa kuacha kukifanya.
Pia thamani ya muda wako itakusaidia kujua majukumu yapi uyafanye na yapi uwape wengine wafanye.
Kwa sasa, kuna majukumu unahangaika kuyafanya, ambayo ni muhimu yafanyike, lakini kuna wengine wangeweza kuyafanya kwa gharama ndogo zaidi.
Chukua mfano wa kufyeka nyasi nyumbani kwako. Ni jukumu muhimu kufanyika. Ukilifanya mwenyewe litakuchukua siyo chini ya saa moja. Ukiweka kibarua wa kulifanya, atakutoza elfu 10.
Sasa hapa ndipo wengi wanapopoteza, anaona elfu 10 ni kubwa, anaweza kufanya kazi hiyo mwenyewe.
Hivyo anaacha kumpa mtu elfu 10 afanye hiyo kazi na kukazana kuifanya mwenyewe.
Anajiona ni shujaa aliyeokoa fedha, ila haoni fedha nyingi alizopoteza kama angemwajiri kibarua afanye kazi hiyo, kisha yeye akatumia muda huo kukamilisha mauzo zaidi.
Jipime kila saa mwa majukumu unayofanya na jiuljze yanachangiaje kwako kufanya mauzo yanayoendana na thamani ya muda wako.
Inaweza isiwe kuuza moja kwa moja, lakini ikawa ni kufanya maandalizi ya mauzo ambayo baadaye yatawezesha kukamilisha mauzo hayo.
Kokotoa thamani ya muda wako na hakikisha chochote unachofanya kinaendana na thamani hiyo ya muda.
Ili uone uchungu wa jinsi unapoteza muda wako mwingi kwa mambo yasiyokuwa na tija, nimekupa utaratibu mwingine.
Utaratibu huo ni kuorodhesha saa kwa saa jinsi unavyotumia muda wako wa masaa 16 kwa siku.
Orodhesha masaa hayo yote, kuanzia saa kumi alfajiri mpaka saa mbili usiku.
Pangilia kila utakachofanya kwenye masaa hayo kulingana na thamanj yake katika kuchangia lengo la mapato.
Rafiki, usijiendee tu kwa mazoea, badala yake pima kila kitu. Namba huwa hazidanganyi, hivyo simama kwenye namba mara zote.
Kama haya mahesabu yamekuvuruga, achana nayo, wewe anza na thamani ya muda wako kuwa ths laki moja kwa saa.
Hivyo chochote unachofanya kiwe kinaingiza laki moja au kuandaa mazingira ya kuweza kutekeleza hilo baadaye.
Kwa mfano kwenye mauzo, unaweza kwa sasa usiwe kufanya mauzo ya laki moja kila saa.
Lakini kama utatumia muda huo vizuri kwenye masoko na mauzo, utaweza kutengeneza wateja tafajiwa wengi zaidi na kuwashawishi kununua.
Anza na namba, kisha utakua kuanzia hapo.
Kama huna namba unazojipima nazo, hakuna namna unaweza kukua.
Na namba ya msingi kabisa ni thamani ya muda wako.
Hiyo ndiyo itaweza kukufungua macho na kukuonyesha wapi unapoteza muda na fedha pia.
Muda ni rasilimali adimu sana, yenye thamani kubwa kuliko hata fedha. Ukipoteza fedha unaweza kuzipata tena, ila ukipoteza muda ndiyo umeupoteza moja kwa moja.
Hivyo badala ya kutumia muda kuokoa fedha, mara zote tumia fedha kuokoa muda.
Maana yake usifanye lolote ambalo thamani yake ni chini ya thamani ya muda wako, hata kama muda unao na fedha huna.
Badala ya kuuchezea muda huo, upeleke kwenye mambo yatakayoweza kukupa thamani kubwa zaidi.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante Sana kocha kwa makala hii, nilikuwa napata shida jinsi ya kukokotoa thamani ya muda wangu. Kwa makala nimeweza kuelewa vizuri.
LikeLike
Thamani ya muda wangu ni 550,000 kwa saa
LikeLike
Kuchezea muda ni kuchezea fedha. Asante Kocha
LikeLike
MASAA 16 YA SIKU.
04:00-05:00 Kusoma meseji za BM na kushiriki amka na BM.
05:00-07:00 Kumsindikiza wife anaenda mkoa.
07:00-09:00 Kuelekea ofisini,kufungua ofosi na kufanya usafi.
09:00-10:00 Kusikiliza tena audio ya BM ya leo.
10:00-11:00 Somo la leo na quiz.
11:00-13:00 Kauli 10 chanya,mambo 16 ya mauzo,maneno ya siku.
13:00-14:00 Lunch.
14:00-16:00 Kuwasiliana na wateja.
16:00-18:00 Kusoma kitabu.
18:00-20:00 Tathmini ya siku,Kufunga ofisi na kurudi nyumbani.
20:00-22:00 Kula,mazoezi na kulala.
LikeLike
Ni kweli kocha Naendelea kuamini kwamba mtu ukiwa unacheza na mahesabu ya kukotoa na kujifanyia tathmini kwa kila jambo linalo fanyika ni rahisi sana mtu kugundua kwamba ni wapi panahitajika maboresho zaidi ya kukua zaidi, kwa mfano mimi binafsi nimekokotoa kwa kuchukua jumla ya mauzo yangu yote kwa mwezi na kugawanya kwa siku 30 nimepata kiasi fulani, harafu pia hicho kiasi nimekigawa pia kwa masaa 16 ambapo nimepata kwamba kwa sasahivi ninafanyia kila lisaa kiasi cha shillingi 4312.5, kitu ambacho nimebaini kwamba ninahitaji kazi ya ziada na kubwa zaidi kwa kukuza mauzo yangu kwa kila lisaa au kutengeneza mazingira wezeshi zaidi ya kuendelea kuongeza kipato changu maradufu
LikeLike
Vizuri,
Ukiboresha ukokotoaji kwenye siku na masaa, hiyo namba itakwenda juu zaidi.
LikeLike
Thamani ya muda wangu ni tsh 100,000 kwa saa.
1. Kuamka kisha kusoma kitabu 04:00-4:25Am
2. Kushiriki kipindi BM 4:30-5:00Am
3. Kusoma kitabu na quiz 5:00-5:30AM
4. Mazoezi 5:30-06:30AM
5. Maandalizi ya kwenda ofisini 06:30-1:30Am
6. Kwenda ofisini 7:30-8:00
7. Kuwapigia simu wateja wapya 8:00-13:00
8. Kuwapigia simu wateja tarajiwa wa zamani 13:00-16:00
9. Kupiga simu kwa wateja ambao walishanunua 16-18:00
10. Kurudi nyumbani
11.kufanya tathimini. 20:00
LikeLike
Kukokotoa thamani ya muda kwa kila saa moja katika masaa 16
Nimegundua kwa Mauzo ninayotakiwa kufanya mwaka 2023 ni tshs (250M) hivyo ukigawanya kwa miezi 12 ni tshs 20M na laki name
20,850,000÷siku 30==tshs 695,000/
Ukichukua hiyo tshs 695,000÷kwa saa16==43,437.5
Kwa mantiki hiyo saa langu moja ni sawa na 43,437.5 ili kufikia lengo la Mauzo ya tshs ((250M)
Nikushukuru kwa kikokotoo iki kutambua thamani ya muda wng kwa saa kuanzia sasa na Kuendelea kuuongeza thamani zaidi kwa kila ninalojiusisha nalo
God bless you kocha
By mwijage vission ((MVFF))
LikeLike
Boresha hapo kwenye siku na masaa, namba itakuwa kubwa zaidi.
LikeLike
Asante kocha nimeweza kulokotoa thamani ya saa moja kwenye siku yangu ya mafanikio.
LikeLike
MATUMIZI YANGU YA MUDA WA SAA 16 LEO TAREHE 12/01/2023
THAMANI YA MUDA WANGU KWA SAA NI 200000/=
(i) Kushiriki Amka## BM -4am-5am
(ii) Kuandika makala kusoma vitabu 5am -6am
(iii) Uandishi wa kitabu-Itawale hasira yako 6am-7:00am
(iv) Kujiambia na kurekodi kauli 10 chanya na kuziaandika + kuandika mambo 16 ya kuzingatia wakati wa mauzo+sheria 13 za mauzo+24 maneno ya ushawishi, Kusoma Bilionea mafunzoni na kufanya quiz 7:00am-8:00am
(v) Kwenda ofsini kufanya kazi- 8:00am -9:00am
(vi) Kukusanya vifaa vya field -9am -10am
(vii) To write the outline for Bagamoyo activity 10am-11am.
(viii) Discussion with Frank on ATSB-11am-12 pm
(ix) Rewrite the ATSB manuscript – 12pm-1 pm
(x) Kujibu emails na mapumziko mafupi ya chakula -1pm-2pm
(xi) Kuandika progress report ya Bohemia project 2:00pm -3:00pm
(xii) Kutembelea wateja -3pm-4pm
(xiii) Kupiga simu 10, kutembelea wateja wateja -4pm-5pm
(xiv) BYU Pathway gathering meeting +assignment on marriage and family studies -5pm – 6pm
(xv) Future Learn Introduction to Psychology week two -6pm-7pm
(xvi) Tathimini ya siku 7pm-8pm.
LikeLike
[16.01.2023] (2022 – 2023)
MGAWANYO WA MATUMIZI YANGU YA MASAA 16
✅ Thamani ya muda wangu kwa sasa ni tsh. 100,000/= kwa 1saa.
04:00Am -5:10Am
-Kufanya ibada, Amka na BM na kuchukua taarifa za msingi kutoka darasani (BM darasani).
5:10Am – 6:10Am
-Kusoma vitabu, kufanya quizes na kusoma makala moja kutoka Kisima Cha maarifa na kuandika nilichojifunza.
6:10Am – 7:00Am
-Kufanya mazoezi na usafi
7:00Am – 8:00Am
-Kwenda ofisini, kunywa chai, kuangalia malengo yangu ya mwaka, mwezi, siku na saa pamoja na vipaumbele vyake.
8:00Am – 9:00Am
-Kusaka wateja wapya na Kufundisha wateja tarajiwa wa zamani kwenye makundi yoote.
9:00Am – 10:00Am
-Kupiga simu kwa wateja tarajiwa wa zamani.
10:00Am – 11:00Am
-Kupiga simu kwa wateja wapya
11:00Am – 12:00Pm
-Kupiga simu kwa wateja wa zamani na wapya, ambao hawakufikiwa.
12:00Pm – 1:00Pm
-Kujibu message za wateja kwenye makundi yote.
1:00Pm – 2:00Pm
-Mapumziko kwa ajili ya chakula na kujiandaa kwa session ya hawamu ya pili jioni.
2:00Pm- 3:00Pm
-Kuweka list ya wateja wa kufatiliwa na kuwatumia mizigo yao mikoani na ndani
3:00Pm – 4:00Pm
-Kupiga simu kwa wateja na kujibu maswali yao
4:00Pm – 5:00Pm
-Kupiga simu kwa wateja wanaohudumiwa na kuwajulia hali
5:00Pm – 6:00Pm
-Kuwapigia simu wateja ambao hawakupokea simu wakati wa session ya asubuhi na jioni
6:00Pm – 7:00Pm
-Kufanya manunuzi niliyopanga kufanya na kufatilia order za watu wa mikoani kama zimeratibiwa vizuri.
7:00Pm : 7:30Pm
-Kufunga ratiba zote za ofisi na kurudi nyumbani.
7:30Pm – 8:00Pm
-Kufanya tathmini ya siku nzima.
#NidhamUpendo
#HakunaChaKunizuia
#LazimaNitoboe
#NitabakiKwenyeMchakatoSikuZoteBilaKuacha
LikeLike
Kaa humu.
LikeLike
Mchanganuo wa Masaa 16
04:00 – 4:10 Kufanya Ibada na Tahajudi na kusoma kitabu cha dini
04:10 – 5:05 Kuandika TDL, Kuandika Maneno ya Ushawishi na kushiriki Amka na BM
05:05 – 06:30 Kujisomea kitabu na kuandika maneni kwenye kitabu, kuandika maneno ya ushawishi, kwenye kitabu na Kujibu Quiz
06:30 – 7:30 Mazoezi & kusikiliza Audio Book na kufuatilia kazi za site na stoo
8:00 – 12:00 Kazini
13:00 -14:00 Kujisomea kitabu kurasa kumi
14:00 -17:00 Kazini
17:00 – 19:00 Kufuatilia maendeleo ya shughuli za site za ukusanyaji kwa siku husika na usakaji, kusoma online course
19:00 – 20:00 Kufanya Tathmini na kujisomea French Vocabury na kuupdate THL
20:00 – 21:00 Kufanya Mawasiliano au Kuwa na familia kama nikiwa maeneo ya nyumbani.
21:00 – 22:00 Kufanya tafakari ya siku na kulala
LikeLike
Ahsante sana Kocha Dr. Makirita Amani.
Thamani Ya Muda Wangu Ni Tsh 100,000/= Kwa Saa.
Nahakikisha chochote ninachofanya kinaendana na thamani hiyo ya muda wangu.
Nalinda Muda Wangu.
Nakaa Kwenye Mchakato.
LikeLike
Simamia thamani hiyo.
LikeLike
Asante kocha,kwa kutuma makara hii ya kukokotoa mda,nimejifunza jinsi ya kujua kila saa moja ninatakiwa kutengeneza sh, ngapi?
Nimechukua mauzo yangu kwa mwaka na kugawa kwa mwezi nagawa kwa wiki na ninagawa kwa siku na pia kugawa kwa saa.
Kwa saa nimepata kiasi cha sh,103,000/= asante.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Ni kweli kabisa kocha,mwanzo nilifikiria kwamba kama sina jukumu la kufanya huo ni muda wa kufurahia kwa sababu muda si kuupa thamani yoyote,ila kwa sasa nikiwa sina jukumu la kufanya najiambia hii ni laki moja naipoteza najikuta natafuta jukumu la kufanya kama kuwapigia simu wateja na kuwasiliana nao.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante kocha nimetambua thamani yangu y muda kwa Kila saa.siku,wiki na mpaka mwezi na MWAKA nikiwa Sina mpangilio mzuri wa muda lazima nitashindwa kufikia malengo yangu kwa kutojali muda na nafasi ninazozipata asanteee.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante kocha nitatumia muda wangu vizuri bila kuuchezea na thamani ya muda wangu ni 100,000 ush kwa li saa
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Badala ya kutumia muda kuokoa fedha, mara zote tumia fedha kuokoa muda.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Badala ya kutumia muda kuokoa fedha basi tumia fedha kuokoa muda.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Muda uheshimiwe na watu wote na matumizi yake kika lisaa kulingana na thaman
LikeLike
Hakika
LikeLike
Muda wangu kwa saa nilishaweka 110,000/= naendelea kupambana maana muda wangu unahitaji mimi niuheshimu na watu wengine wauheshimu pia.
LikeLike
Safi sana, komaa kwenye hilo.
LikeLike
Usifanye lolote lenses thamani chini ya muda
LikeLike
Kabisa.
LikeLike