2940; Namba mbaya kwenye biashara.
Rafiki yangu mpendwa,
Ipo namba ambayo ni mbaya sana kwenye biashara na ambayo unapaswa kuiepuka kama unataka kujenga biashara yenye mafanikio makubwa.
Namba hiyo ni moja.
Kuwa na kitu chochote kimoja kwenye biashara ni hatari kubwa.
Inakuweka kwenye utegemezi mbaya na unaokuwa kikwazo kwa ukuaji.
Usiwe na mfanyakazi mmoja pekee kwenye biashara, kwani akikuambia anaacha kazi, biashara yako itaathirika sana.
Kuwa na mfanyakazi zaidi ya mmoja ili lolote linalotokea kwa mmoja lisiathiri biashara.
Tukiwa hapo kwa wafanyakazi, asiwepo mfanyakazi mmoja pekee ambaye ndiye anaweza kufanya kitu fulani. Bali kila kitu kiweze kufanywa na mfanyakazi zaidi ya mmoja. Hiyo itaondoa kukwamishwa pale mmoja anapokuwa na changamoto, kwani mwingine anaweza kufanya majukumu yake.
Usiwe na mteja mmoja pekee au anayetegemewa sana na biashara. Kwani mteja huyo akisema anaondoka, biashara inatikisika sana. Au hata akitaka mabadiliko ya bei, biashara haitakuwa na namna bali kukubali, kwa kuwa ina utegemezi mkubwa kwake.
Jenga biashara yenye wateja wengi na hata mteja awe mkubwa kiasi gani, kuondoka kwake kusiathiri sana biashara.
Hili ni muhimu kuzingatia, kwa sababu ni rahisi kujisahau kutafuta wateja wapya pale unapokuwa na mteja mmoja au wachache wakubwa wanaoleta faida kubwa.
Usipate usingizi kama biashara yako inategemea mteja mmoja.
Usiwe na njia moja tegemezi ya kufanya chochote kwenye biashara. Iwe ni masoko, mauzo, kuajiri n.k. Kama kuna njia moja pekee unayotegemea kwenye kukamilisha mambo muhimu kwenye biashara, utajikwamisha. Kwa mfano kama njia pekee ya kupata wateja ni matangazo kwenye mitandao ya kijamii, siku ikitokea shida kwenye njia hiyo unakosa kabisa wateja.
Usiwe na kifaa kimoja cha msingi kwenye biashara, ni kujiweka kwenye hali ya kukwamishwa haraka.
Kwa mfano kama biashara yako inahusisha matumizi ya kompyuta kama zana kuu, usiwe nayo moja. Kwani inapoharibika au kuwa na changamoto, itaathiri sana biashara.
Kadhalika simu, gari, mashine ya kuchapa na vifaa vingine, kama ndiyo cha msingi kabisa kwenye biashara, kiwepo zaidi ya kimoja.
Hata kama humilili vifaa hivyo, angalau uweze kupata kifaa cha kutumia pale unapokuwa na uhitaji.
Hakuna kitu ambacho huwa kinanishangaza kama mwandishi ambaye ana kompyuta moja pekee.
Na mbaya zaidi, kazi zake zote zinakuwa ndani ya kompyuta hiyo.
Ni kujiandaa kukwamishwa, maana kuna siku kompyuta hiyo itasumbua na utaweza kupoteza kila kitu.
Kwa mwandishi, hata kama huwezi kumudu kuwa na kompyuta zaidi ya moja, basi usiache kazi zako kwenye kompyuta moja. Badala yake hifadhi kazi zako zote kwenye mtandao, kiasi kwamba ukitumia hata kompyuta ya mtu mwingine utaweza kuzifikia na kuendelea kuzifanyia kazi.
Kuwa na utegemezi kwenye kitu chochote kimoja kibiashara ni kujiandaa kushindwa. Kwani kitu hicho kimoja unachokitegemea huwa kinakuangusha pale unapokuwa na uhitaji mkubwa.
Kwenye maeneo yote muhimu ya biashara yako, kuwa na kitu zaidi ya kimoja unachotumia, hata kama siyo vyote unavyomiliki wewe.
Unachopaswa kuepuka ni usikwamishwe na chochote kinachoshindwa kwenda vile kinavyopaswa kwenda.
#NidhamuUandilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha. Hili nalifanyia kazi. Nahakikisha kwamba siwi na mfanyakazi mmoja ambaye namtegemea. Kwenye hili nipo nalifanyia kazi ili niweze kupata mfanyakazi mwingine wa ziada ambaye atakuwepo kwenye biashara na ataanza kazi mara moja.
Kwenye masoko, sitategemea kupata wateja kwa njia ya mtandao tu. Nitahakikisha kwamba nakuwa na njia mbadala.
Kwenye vifaa vya kazi, kwa sasa nina kompyuta moja. Ila hili nalifanyia kazi kuhakikisha kwamba nakuwa na kompyuta nyingine kufikia mwezi wa sita. Sambamba na hilo nitaongeza simu mbili za ziada ya kazi.
Moja kwa ajili yangu, nyingine kwa ajili ya mfanyakazi nitakayemleta kazini siku za karibuni.
Kwa upande wa wateja, nafanyia kazi mchakato wa kuwa na wateja wengi. Wateja wa kawaida mpaka wateja wakubwa.
Asante
LikeLike
Ahsante sana sana Kocha Dr Makirita Amani.
Hii message imenikumbusha mbali sana na nitahakikisha nalifanyia kazi.
Ni kweli kitu kimoja kinaathiri biashara hasa kuwa na mfanyakazi mmoja ambaye ndo ana uwezo pekee wa kufanya kitu fulani.
Ahsante sana
#NidhamUpendo
LikeLike
Epuka sana namba moja
LikeLike
Ahsnate sana kocha, daaah hii makala ni ya moto sana, kuanzia leo nakwenda kuhakikisha kuwa kwenye maeneo muhimu sitegemei kitu kimoja.
LikeLike
Asante kocha kwa kuelezea hii namba moja na ubaya wake, hakika nitaendelea kuifanyia Kazi ili kujiondoa ktk utegemezi na kujiandaa kushindwa wakati naamini”Mimi ni mshindi na nitaendelea kushinda ktk kila changamoto nitakayokutana nayo.
LikeLike
Namba mbaya kwenye biashara…
LikeLike
Hii makala kocha ni kama umeniandikia mimi,nitahakikisha nakuwa na vifaa viwili viwili vya kazi has ktk ofisi yangu ya stationery.
LikeLike
Ukitegea njia moja, mteja mmoja, mfanyakazi mmoja, kila kitu kama huna mbadala ni rahisi kuañguka.
Kuanzia leo nakwenda kuweka mpango wa kuwa na vitu ninavyotegemea kwenye biashara yangu zaidi ya kimoja.
LikeLike
Asnate Sana Kocha kwa makala hii. Imeniamsha na kunipa tahadhari kuwa, kumtegemea mtu mmoja au kitu kimoja kwenye biashara ni hatari Sana. Majukumu ya Msingi ambayo ni roho ya biashara nitayaanisha na kuweka mbadala kuhakikisha mikwamo isiyokuwa ya lazima inaepukika.
WAHUDUMIAJI zaidi ya wawili
WASAKAJI zaidi ya wawili
Bidhaa za kutosha na mfumo wa kutengeneza na kufatilia wateja.
LikeLike
Asante sana kocha Kwa makala hii,kwangu yameshaanza kutokea sasa hivi Nipo Dukani mwenyewe wafanyakazi wote hawapo mmoja kakimbia mwenyewe baada ya kuona kazi ni gumu na mwingine amepata matatizo ya ugonjwa wa UTI sasa ni wiki mzima, baadhi ya kazi zimesimama na Nipo peke Yangiu Dukani
Sasa hii makala inanihusu kabisa Somo kubwa hapa ni kujitafakari na kuchukua hatua
Asante
LikeLike
Asante kocha kwa somo hili la kutokua tegemezi kwenye kitu kimoja
Najitajid kwenye biashara yangu niweze kuwa na mbadala wa kila kitu ili kuepuka kukwamishwa napokua na utegemezi wa kotu kimoja
LikeLike
Sahihi kochà kutegemea kitu kimoja ni hatari sana mara nyingine huwa nawaza hivi intanet ikifungwa tunapata wapi mbadala?
LikeLike