2966; Kwa nini usiwe wewe?
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa mambo yote makubwa unayotaka kufanya au kufikia, tayari kuna wengine wanafanya au wameshafikia.
Swali kubwa unalopaswa kujiuliza ili likusukume ni kwa nini na wewe pia usiwe?
Kuna vipindi ambavyo watu huwa wanalalamikia sana biashara. Uchumi unakuwa mgumu na wateja wanakosa nguvu ya kununua.
Lakini hata mambo yawe magumu kiasi gani, kuna wateja wanaoendelea kununua, tena kwa wingi.
Swali muhimu sana unalopaswa kujiuliza na kujijibu ni kwa nini wasinunue kwako?
Hii dunia ina mabilionea wengi sana.
Afrika pia inao mabilionea wengi.
Tanzania tuna bilionea mmoja anayejulikana kwa viwango vilivyo wazi.
Kama kumeweza kuwepo hao mabilionea, hasa kwa mazingira ambayo na sisi pia tupo, swali ni kwa nini na wewe usiwe mmoja kati ya mabilionea hao?
Katika siku yoyote ile, kuna watu wananunua bidhaa au huduma unayouza, watu ambao unao uwezo wa kuwafikia na kuwahudumia.
Swali ni kwa nini watu hao wasipate mahitaji yao kwako?
Nikujibu kwa nini hutakuwa wewe.
Sababu kubwa kabisa ni hutaki.
Ndiyo, hutaki tu.
Najua unaweza kuwa unabisha, kwa kutoa sababu na visingizio mbalimbali.
Lakini mwisho wa siku ukweli unabaki kwamba huwi wewe au hupati kwa sababu hujataka hasa kutoka kwenye moyo wangu.
Sitaki nitumie nguvu na muda mwingi kukushawishi kwenye hili.
Nataka upitie mifano yako mwenyewe, angalia vitu vyote ambavyo umewahi kuvitaka sana kwenye maisha yako, lakini ukakutana na magumu na changamoto katika kufanyia kazi.
Kwa kuwa ulikuwa unataka sana, hukukatishwa tamaa, badala yake ulipambana kweli na mwishowe ukapata ulichotaka.
Kwa upande wa pili, kuna vitu unakuwa umetamani kuvifanya au kuvipata, lakini hujajitoa hasa.
Kwa vitu vya aina hiyo umekuwa unakutana na magumu na changamoto mbalimbali, ambazo umekuwa unazikubali kama kikwazo.
Somo kubwa tunalopata hapa ni kupata au kukosa tunachotaka inaanzia ndani yetu wenyewe.
Mambo ya nje yana mchango mdogo sana.
Maamuzi hasa na matokeo yanaanzia ndani.
Kama mtu anakitaka kweli kitu na hayupo tayari kutokukipata, lazima atakipata. Inaweza kuchukua muda mrefu, lakini mwisho anakipata.
Magumu, vikwazo na changamoto huwa ni kikwazo halisi kwa wale ambao hawajajitoa hasa kupata wanachotaka.
Lakini kwa wale waliojitoa hasa, ambao wameamua watapata wanachotaka hata iweje, hakuna kinachowazuia.
Chochote kinachopita kwenye njia yao, kinakuwa sababu ya wao kufika kule wanakotaka kufika.
Je wewe umejitoa kiasi gani kuhakikisha unapata kweli kile ulichodhamiria kweli kukipata?
Je umejihakikishiaje kwamba hata kama wateja wanaonunua ni wachache, basi wananunua kwako?
Unaweza kuwa na kupata chochote unachotaka kama utaamua kweli kukipata na kujitoa kwa kila namna kuhakikisha kweli kwamba unakipata.
Usikubali kuyumbishwa, jua kile hasa unachotaka na inyeshe mvua au liwake jua, lazima upate unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante kocha,mimi ndo mwenye maamuzi ya maisha yangu iwe mvua au jua inabidi nifanye kazi kwa bidii ili nitimize ndoto yangu sio kuweka visingizio.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ahsante sana kocha
LikeLike
Karibu
LikeLike
Inyeshe mvua ama litoke jua nitapigania minachokitaka
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Asante Kocha kwa hakika kinachotuzuia ni hitaji la moyo la ndani kila kitu kinawezekana kwanini mimi Isaack inside bilionea kama Dewji ameweza kwenye mazingira haya haya haiitaji upendeleo ila kujitoa kweli.
LikeLike
Tuanzie hapo na mengine yatakwenda sawa.
LikeLike
Nitapata ninachokitaka,iwe jua au mvua.Nitapitia magumu lakini nijue hiyo ni kawaida niwe na msimamo kufika nilipoamua.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Kujua kile unachokitaka ni hatua Muhimu sana katika kufikia kwenye kilele cha mafanikio na ndio jambo kubwa sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
…..ATTITUDE…. Kwa MTAZAMO CHANYA mambo yanawezekana, penye magumu ndipo ilipo fursa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hakika!
LikeLike
Magumu, vikwazo na changamoto huwa ni kikwazo halisi kwa wale ambao hawajajitoa hasa kupata wanachotaka.
Lakini kwa wale waliojitoa hasa, ambao wameamua watapata wanachotaka hata iweje, hakuna kinachowazuia.
Chochote kinachopita kwenye njia yao, kinakuwa sababu ya wao kufika kule wanakotaka kufika.
LikeLike
Hakika.
Na dunia huwa inamjaribu kila mtu kuona amejitoa kiasi gani.
LikeLike
Kupata au kukosa tunachotaka inaanzia ndani yetu wenyewe. Asante kocha
LikeLike
Kabisa,
Unaanza na ushindi ndani kisha kwenda kudhihirisha uwanjani.
Tuanze na ushindi ili tusikubali kupoteza.
LikeLike
Ni kweli kabisa ukiamua kupata chochote unacnachotaka utakipata
Asante
LikeLike
Ni kuamua tu na kukataa kukata tamaa.
LikeLike
Nimeshaamua, nitaupata Ubilionea au nitakufa nikiutafuta, chaguo ni langu na muda ni Sasa. Ndiyo Mimi ni Bilionea, naitafuta Kama pumzi na Niko tayari kulipa gharama. Nitabakia kwenye mchakato mpk niupate.
LikeLike
Kaa humu na lazima iwe.
Hakuna namna.
LikeLike
Iwe mvua au jua lazima nipate ninachotaka.
LikeLike
Safi sana.
Dunia haiwezi kukukatalia kama utakataa kukata tamaa.
LikeLike
Unapata kile unachotaka kama ukiamua kukipata wewe mwenyewe kutoka ndani ya moyo wako.
Asante sana
LikeLike
Maamuzi ya ndani ndiyo yenye nguvu kuliko chochote cha nje.
LikeLike
Napambana kupata ninachokitaka liwake jua inyeshe mvua sipaswi kukata tamaa
LikeLike
Kukata tamaa ni dhambi kubwa na usaliti mbaya kwako mwenyewe.
LikeLike
Kila kikwazo na ugumu inayokuja katika njia yangu ni kichocheo tuu Cha kunifikisha ninapotaka (nataka haswaa) kwenda na si vinginevyo…hakuna Cha kunizuia lazima nitoboe
LikeLike
Kataa chochote ambacho siyo kile unachotaka.
Maana dunia haikupi unachostahili, bali inakupa unachokubali.
Usikubali chochote chini ya unachotaka hasa.
LikeLike
Asante Sana kocha, nahitaji kupambana tu,KWa nini nisiwe mimi kwenye kile ninachotaka,itanisukuma zaidi,
LikeLike
Ukishaamua na kutia nia ya kweli, lazima uwe, hakuna cha kukuzuia.
LikeLike
Najiona kuwa bilionea ninayefuata baada ya Mohamed Dewji,
Nitapambana usiku na mchana kufanikisha hilo.
LikeLike
Hiyo imekuwa.
Umeshakiri,
Kilichobaki ni kufia kwenye hilo.
Usikubali kuyumbishwa,
Usikubali kuzembea.
LikeLike
Sikubali kuyumbishwa, najua kile hasa ninachotaka na inyeshe mvua au liwake jua, lazima nipate ninachotaka.
Ahsante Kocha.
LikeLike
Komaa kwenye hilo.
LikeLike
Jua liwake mvua inyeshe haijalishi ni muhimu kukomaa
LikeLike
Hakuna kukata tamaa mpaka tupate kile tunachotaka.
LikeLike