3111; Kazi yako kuu.
Rafiki yangu mpendwa,
Mimi siyo Mkatoliki na wala sifungamani na dini yoyote, lakini kuna ujumbe nimekutana nao mtandaoni kuhusu Wakatoliki na nimeona kuna mengi sana ya kujifunza kwenye hii safari yetu ya mafanikio makubwa.

Ujumbe huo, unaeleza kama ifuatavyo;
“Ninapenda sana kiwango cha Wakatoliki cha kutokusumbuka. Utakosoa dini yao, watakusikiliza mpaka umalize. Wataenda kanisani, watakula sakramenti, watapita baa yao pendwa na kunywa bia wanayopenda kisha kurudi nyumbani. Hawapotezi nguvu zao kutetea dini yao. Hawajisumbui hata kuangalia kama unavaa nguo ile ile kila jumapili.
Hawana hata vipaza sauti nje ya makanisa yao kuwasumbua watu wengine, hawafanyi hata mikutano ya injili. Ukitaka kujiunga nao, unaenda kanisani kwao. Hawana muda wa kuhubiri dhidi ya madhehebu mengine. Hawana hata muda wa kupoteza kwenye utambulisho wa wageni kwa salamu zisizo na umuhimu. Kujali mambo yao ndiyo kazi yao kuu.
Ni dhehehu lenye nidhamu ya hali ya juu sana.”
Kama nilivyosema, ukiutafakari ujumbe huo nje ya dini, kuna mambo mengi sana unajifunza ambayo ukiyatumia kwenye hii safari ya mafanikio makubwa, yanakuwa na tija kubwa.
Baadhi ya mambo hayo ni kama ifuatavyo;
1. Umuhimu wa kuwa na Mfumo.
Ukiangalia yaliyoelezwa kwenye huo ujumbe, utaona wazi kwamba nguvu iliyopo kwenye Kanisa Katoliki ni mfumo mzima wa kuendesha kila kitu.
Pamoja na wingi wa makanisa hayo, yote yanaendeshwa kwa namna moja, kwa sababu yanatumia mfumo mmoja.
Ni muhimu sana tuwe na mifumo ya kuendesha biashara zetu ili kila kitu kifanyike kwa usawa hata kama sisi wenyewe hatupo kwenye biashara moja kwa moja.
2. Kujali wale ulionao tayari.
Ujumbe unaonyesha jinsi ambavyo kanisa linatoa huduma kwa waumini ambao tayari linao. Ni kupitia huduma nzuri kwa waumini hao ndiyo linategemea kukua zaidi. Kanisa halitumii nguvu kubwa kuvuna waumini wapya, badala yake linakazana kuwabakisha wale waliopo ili familia zao zibaki na waweze kuwavutia wengine.
Ni muhimu sana uwajali na kuwahudumia vizuri wateja ambao tayari unao kwenye biashara yako, ili waendelee kubaki na pia wakuletee wateja wengine wapya.
Ni rahisi sana kuendelea kumuuzia mteja ambaye tayari yupo kuliko mteja mpya. Pia wateja wanaoletwa na wateja ambao tayari unao, huwa ni rahisi kuwashawishi wakubali kununua.
Hivyo nenda vizuri na wateja ambao tayari wananunua kwako, huo ni mgodi wa dhahabu wa biashara yako.
3. Kutokuhangaika na wakosoaji.
Haijalishi unafanya kitu gani, kuna watu watachagua tu kukukosoa. Watakuonyesha jinsi ambavyo unakosea na haupo sahihi. Watakushauri namna bora ya kufanya.
Lakini unachopaswa kufanya ni kama ujumbe unavyoeleza kwa Wakatoliki, puuza na endelea na mambo yako.
Wasikilize wakikukosoa na kukukatisha tamaa, halafu wakimaliza wewe endelea kujenga biashara yako kwa namna ambavyo umechagua kuijenga.
Kama ambavyo nimekuwa naeleza, usisikilize wala kuchukua ushauri ambao watu wanakupa bila ya wewe kuwaomba wakushauri.
Watu huwa ni rahisi kushauri, ila hawajui jinsi viatu ulivyovaa vilivyokuwa vigumu.
4. Kutohangaika na washindani.
Tumekuwa tunajifunza hili mara zote, njia bora ya kuwashinda washindani siyo kushindana nao, bali kuwa bora zaidi kwenye kile unachofanya.
Usipoteze muda wako kuangalia washindani wanafanya nini au unawazidije, badala yake peleka muda huo kufikiria unawapaje thamani kubwa zaidi wateja ambao tayari unao.
Kadiri unavyowapa wateja thamani kubwa wasiyoweza kuipata mahali pengine, ndivyo unavyokuwa mbele zaidi ya ushindani, bila hata ya kushindana moja kwa moja.
5. Matumizi sahihi ya nguvu na muda.
Nguvu na muda ni rasilimali zenye uhaba na ukomo mkubwa. Ukitumia rasilimali hizo kwenye mambo yasiyokuwa na tija, unashindwa kufanya yale yenye tija.
Kama ambavyo ujumbe unaonyesha Wakatoliki hawahangaiki na yasiyokuwa muhimu, ndivyo pia na wewe hupaswi kuhangaika na yoyote yasiyokuwa muhimu kwa ukuaji wa biashara yako.
Kazi yako kuu ni kujenga biashara yako, hiyo ndiyo kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako.
Kwa kila unachotaka kufanya, jiulize kina mchango gani kwenye ukuaji wa biashara. Kama hakina mchango, achana nacho mara moja.
6. Ni sahihi na siyo sahihi.
Kitu kimoja ambacho nadhani Mapadri wa Kikatoliki wamefundishwa kwenye masomo yao ya muda mrefu ni kwamba kuna vitu ambavyo ni sahihi kwenye Ukatoliki na kuna ambavyo siyo sahihi.
Hivyo badala ya kuangalia visivyo sahihi, wao wanaegemea kwenye vile vilivyo sahihi.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye biashara zote, kila biashara ni sahihi na siyo sahihi.
Kuna vitu vizuri kwenye kila aina ya biashara, halafu kuna vitu ambavyo pia siyo vizuri.
Ukiwa unaangalia ni vitu gani vibaya kwenye biashara na kisha kuacha na kwenda kwenye nyingine, hakuna biashara ambayo utadumu nayo kwa muda mrefu.
Chagua biashara unayotaka kufanya na angalia mazuri yake zaidi, angalia usahihi wake na achana na mapungufu yake.
Muhimu ni kujenga biashara inayokufikisha kwenye ndoto zako na siyo kuangalia ukamilifu wa biashara.
7. Nguvu ya jumuia.
Moja ya vitu ambavyo Kanisa Katoliki pamoja na dini nyingine zimeona kina nguvu ni jumuia.
Licha ya kuwepo kwa kanisa ambalo linawaleta waumini wote pamoja, kuna jumuia ambazo zinawaweka waumini karibu zaidi. Waumini hao wananufaika zaidi na jumuia zao kuliko hata wanavyotegemea kunufaika na ahadi ambayo dini inawapa kwenye maisha yajayo.
Kujenga biashara imara na yenye wateja waaminifu, jenga jumuia ya wateja wa biashara yako. Wafanye wateja wanufaike zaidi kupitia jumuia hiyo kuliko hata wanavyonufaika na kununua kile biashara inauza.
Ukiweza kuwapa wateja thamani kubwa kwenye jumuia, washindani watakuwa na wakati mgumu sana kukuibia wateja wako.
Ila kama wapo wapo tu, inakuwa rahisi kuchukuliwa na washindani.
8. Nidhamu ya hali ya juu.
Jambo la mwisho muhimu tunalojifunza kwenye ujumbe huo ni nidhamu ya hali ya juu sana ambayo kanisa na waumini wanayo. Hiyo pia ndivyo ilivyo kwenye dini zote na falsafa zote.
Kwenye Ukristo kuna ibada ambazo waumini wanapaswa kushiriki na sakramenti mbalimbali ambazo ni lazima wapate. Kuna masharti ya mtu kutimiza ili apate yote hayo na wanayatimiza.
Kwenye Uislamu kuna sala tano kila siku ambazo mtu anapaswa kuzitimiza na kuna mwezi wa mfungo kwenye kila mwaka, pamoja na taratibu nyingine ambazo ni lazima zifuatwe.
Dini hizo haziwaambii waumini wake wakipenda wafanye wasipopenda wasifanye, badala yake zinaelekeza hayo ni lazima kufanyika na yanafanyika kweli.
Unapaswa kuwa na nidhamu ya juu sana kwenye uendeshaji wa biashara yako.
Wafanyakazi wote waliopo kwenye biashara yako kuna mchakato ambao lazima waufuate kwenye kutekeleza majukumu yao. Huo siyo mchakato ambao wanafanya pale wanapojisikia, bali wanapaswa kuufanya mara zote bila kukosa.
Kadhalika wateja wanapaswa kujengewa nidhamu wanayotakiwa kuwa nayo kwenye biashara yako. Kuna vitu wanavyotakiwa kufanya kila wanapokuja kwenye biashara yako na kuvizingatia bila kukosa.
Kwa kujenga nidhamu ya aina hiyo kwenye pande zote mbili, kuendesha biashara yako inakuwa kitu chenye raha kubwa kwako.
Rafiki, kama nilivyokuambia, ukiondoa dini kwenye huo ujumbe, kuna mengi sana ambayo unajifunza na ukiyafanyia kazi kwenye safari yako ya mafanikio, utapata manufaa makubwa.
Kwa vyovyote vile, kitu chochote ambacho kimeweza kudumu kwa miaka zaidi ya 500, lazima kuna vitu inakuwa inafanya kwa usahihi.
Hivyo ndivyo ukijifunza na kuvifanya, utaweza kupata matokeo bora pia.
Nenda katumie haya uliyojifunza uweze kujenga biashara kubwa, yenye mafanikio na isiyokutegemea moja kwa moja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwa hakika lazima kujenga biashara yenye mfumo imara unaofuata kanuni sahihi zinazoendesha mfumo huo.
LikeLike
Hapo ndipo penye uimara.
LikeLike
Somo kubwa sana la kujifunza kupitia ujumbe huu, hongera sana Kocha Dr Makirita Amani kwa kuandika vizuri ujumbe huu kwa uhalisia kwenye biashara.
LikeLike
Asante sana, tuna mengi ya kujifunza kila kona, ni sisi kuwa tayari kufungua macho na kujifunza.
LikeLike
Asante kocha Kwa ujumbe huu kwenye biashara zetu.
Ni kweli kabisa tukiweza kujenga jumuia Bora kwenye biashara zetu hatutakuwa na hofu ya kupoteza wateja.
Hakika jumuia ni Moja ya njia Bora ya kufanya wateja wafaidike zaidi na hapo biashara itakuwa zaidi.
Kupitia ujumbe huu wa kanisa Katoliki nimeona fursa kubwa itakayokuja kunufaisha familia zetu kupitia jumuia ya kisima Cha maarifa.
LikeLike
Asante na karibu sana.
Ni kweli, kazi kubwa ya kila mmoja wetu ni kujenga hii jumuia ya KISIMA CHA MAARIFA ili ije kuwa na manufaa kwa vizazi vyetu vingi vijavyo.
LikeLike
Nimejifunza kitu kuhusu ukatoliki
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
Asante Kocha kwa ujumbe huu mzuri. Mfumo ni muhimu na unanguvu sana kwenye biashara zetu. Unafanya tusihangaike na mambo mengine yasiyo ya msingi kwenye biashara.
LikeLike
Hakika, tujenge mfumo imara na tuufuate huo.
LikeLike
Kabisa misingi hii ni Bora na ukiifiuata lazima utakuwa na matokeo makubwa
Asante sana
LikeLike
Hakika, tukae kwenye misingi na kitakachobaki ni muda tu.
LikeLike
Asante sana kocha. Mfumo una nguvu kweli. Kwenye Ibada kanisa katoliki lina mfumo ambao unafahamika. Iwe upo tanzania au nje ya Tanzania.
Ibada zote zinaendeshwa kwa mfumo huohuo….
Hiki ndicho kitu ambacho nakifanyia kazi kwenye biashara yangu. Mfumo. Mfumo. Mfumo
LikeLike
Mfumo una nguvu sana, tukifanikiwa hapo, tumefanikiwa yote.
Tuweke kazi kubwa kwenye kujenga mfumo, huo ndiyo utakaotuweka huru.
LikeLike
Asante sana kocha
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante Kocha,
Nguvu na muda ni rasilimali adimu sana. Ili ninufaike nitakuwa na mfumo imara na nidhamu kali.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kwa vyovyote vile, kitu chochote ambacho kimeweza kudumu kwa miaka zaidi ya 500, lazima kuna vitu inakuwa inafanya kwa usahihi.
Hivyo ndivyo ukijifunza na kuvifanya, utaweza kupata matokeo bora pia
LikeLike
Kabisa
LikeLike
ASANTE sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kutojali na kuhangaika na wakosoaji.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakika,kazi yangu kuu ni kuyaweka haya kwenye matendo. Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ni kweli ni muhimu kujenga jumuia ya wateja na kuwa karibu nao iliuweze kuwapa thamni kubwa na kuwazuia kuibiwa na wengine
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Hata mimi siyo mkatoliki. Hapa nimeweka dini pembeni na nimejifunza kanuni kubwa sana katika ujumbe huu.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi uliyojifunza.
LikeLike