3181; Tuko hapa kwa ajili ya utekelezaji.
Rafiki yangu mpendwa,
Kipindi cha nyuma, maarifa yalikuwa adimu sana kiasi cha watu kuwa tayari kuwa tayari kulipa gharama kubwa ili kuyapata na kuyatumia kupiga hatua kubwa.
Kadhalika kwa mawazo mazuri ya biashara na miradi mingine.
Kuna watu waliweza kuingiza kipato kikubwa kwa kuuza tu mawazo ya biashara au ushauri mwingine wa aina hiyo.
Lakini kwa sasa mambo yamebadilika sana.
Maarifa yanapatikana kwa wingi na urahisi sana.
Mawazo ya biashara ndiyo usiseme, ni mengi na ya bure kama hewa tunayopumua.
Na kwa upande wa ushauri, watu wanapewa ushauri mwingi kabla hata hawajauomba.
Mabadiliko hayo yanafanya biashara ya maarifa, mawazo na ushauri kukosa thamani.
Watu wanakuwa hawapo tayari kulipa gharama kubwa kupata vitu hivyo ambavyo wanaweza kuvipata bure au kwa gharama ndogo.
Pamoja na bahari ya upatikanaji mkubwa wa maarifa tuliyopo, bado watu wana kiu kubwa sana ya mafanikio.
Yaani ni sawa na mtu kufa kwa kiu wakati yupo kwenye ziwa kubwa na lenye maji safi kabisa.
Au kufa kwa njaa wakati yupo kwenye jiko lenye kila aina ya chakula.
Pamoja na wingi na urahisi wa kupatikana kwa maarifa, mawazo na ushauri, mafanikio yamezidi kuwa magumu kwa watu wengi.
Watu wamekuwa wanabeza kwa nini unakuta mtu anauza kitabu kinachoitwa jinsi ya kuwa tajiri wakati wao ni masikini. Kwa nini wasisome vitabu hivyo wao wenyewe na kuwa matajiri?
Au unakuta mtu ameandika kitabu cha jinsi ya kupata mtaji wa kuanza biashara, lakini anakosa fedha za kukichapa. Kwa nini wasisome kitabu walichoandika na wakapata fedha za kukichapa?
Ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba maarifa pekee kwa sasa hayatoshi.
Kila mtu anaweza kupata maarifa yoyote anayoyataka.
Kwa sasa kitu chenye thamani kubwa ni utekelezaji wa maarifa, mawazo na ushauri mbalimbali.
Hilo la utekelezaji ndiyo linalotukutanisha hapa na kutuweka pamoja.
Wakati tunaanza, maarifa ndiyo yalikuwa yanatukutanisha.
Tulikuwa wengi, kwa sababu watu waliyafurahia maarifa mazuri waliyoyapata.
Kwenye kanuni yetu ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO, tuliegemea zaidi kwenye maarifa.
Na watu walifurahia sana, kupata maarifa ya kipekee ambayo hayapatikani kwingine kwa urahisi.
Lakini hakukuwa na hatua kubwa walizokuwa wanapiga na hivyo hata kulipia huduma ikawa vigumu kwao.
Tulipoanza kusisitiza upande wa VITENDO yaani kuchukua hatua ya utekelezaji, ndiyo watu wakaanza kukimbia kimbia.
Na mpaka sasa bado watu wanakimbia kimbia.
Kila tukibonyeza kutaka utekelezaji zaidi, kuna watu wanakimbia.
Na hakuna namna tutaacha hilo.
Maana ndiyo namna pekee ya kila mmoja kupata thamani.
Kulazimishwa kufanya vitu ambavyo hutaki kufanya, ili kupata matokeo makubwa ambayo hujawahi kuyapata.
Hivyo kitu kimoja ambacho nakuahidi bila kupepesa macho ni mchezo ndiyo kwanza unaanza.
Huu mchezo hauna mwisho.
Ni mchezo wa kukaa kwenye mchakato na kutekeleza kwa uhakika, iwe unataka au hutaki.
Ni mchezo ambao hauna fainali au kuhitimu, kila wakati ni kuchukua hatua kubwa na za juu zaidi, kwa ukubwa, bila hofu na bila sababu.
Unaweza kujificha nyuma ya sababu mbalimbali, lakini muda ni mwalimu mzuri, utachemka tu.
Tupo hapa kutekeleza, hatua kwa hatua mpaka kila mtu afikie malengo yake makubwa.
Kwa kila atakayekaa hapa na kutekeleza kwa uhakika bila hofu au sababu, lazima atatafikia malengo makubwa aliyonayo.
Huo ni uhakika na siyo kubahatisha.
Lakini hilo halitatokea kwa kutaka uende vile unavyojisikia wewe mwenyewe.
Litatokea kwa kukubali kukaa kwenye mchakato na kuutekeleza kwa uhakika bila kuyumbishwa na chochote kile.
Unaweza kukaa hapa kwa kuzuga na kujificha nyuma ya maneno na visingizio mbalimbali.
Unaweza kuwa mzuri kwenye kujifunza na ahadi.
Lakini kama hutekelezi kama programu inavyotaka ufanye, utachemka tu.
Na wala hatuna haraka kwenye hilo, ni swala la muda tu, ambao utaweka kila kitu hadharani.
Baada ya muda, utaweza kuonyesha matokeo au ukatoa sababu.
Na sababu hazitakuwa na tija.
Hivyo basi, nitoe wito, ambao nimekuwa nautoa mara kwa mara lakini bado watu hawaupi uzito.
Kaa hapa kama kweli umejitoa katika kutekeleza haya tunayojifunza na kushirikishana.
Kaa hapa kama upo tayari kutekeleza hata kama hujisikii kufanya hivyo.
Kama unataka tu kufurahia maarifa, kujisikia vizuri kwa yale unayojifunza, upo mahali ambapo siyo sahihi tena kwako.
Na patakutesa sana.
Amua leo, kama utakaa hapa na kutekeleza kwa viwango vya juu sana, bila ya hofu wala sababu.
Au la, achana na hii kitu, jiweke pembeni na endelea kufurahia maarifa mengi ambayo mpaka sasa tayari umeshayapata.
Hakuna katikati, hakuna vuguvugu, ni unakuwa moto sana kupitia utekelezaji na kuendelea kuwa hapa, au unakuwa baridi kabisa kwa kutokutekeleza na kukimbia.
Ni unaenda kwa ukubwa (go big) au unaenda nyumbani (go home).
Chagua upande na kaa kwenye huo upande.
Mguu mmoja nje na mguu mwingine ndani ni hatari kubwa kwako, usijaribu hilo.
Kama umechagua kukaa hapa, umechagua kutekeleza kwa uhakika, ukubwa, bila hofu na bila sababu.
Na siyo kitu kingine chochote.
Unapoambiwa uonyeshe ushahidi wa utekelezaji wako na kuanza kukimbia kimbia, tunajua ulikuwa umepotea njia.
Hakuna namna unaweza kujificha tena, hakuna sababu itakayokusitiri tena.
Ni utaonyesha unafanya au hufanyi.
Imani yangu ni utachagua kwa usahihi, kukaa hapa na utekeleze hasa au kujiweka pembeni.
Maisha ni kuchagua.
Na kuna wakati utalazimika tu kuchagua.
Iwe unataka au hutaki.
Hivyo ni bora kuchagua sasa.
Ili usipoteze muda wako kwa namna ambayo haina tija.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hongera sana Kocha kwa kuendelea kusimamia kanuni ya KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO. Nimechagua kukaa hapa kwa kutekeleza yale yote yanayopaswa kufanyika kupitia mchakato wa bilionea mafunzoni.
Asante sana.
LikeLike
Vizuri sana.
Karibu.
LikeLike
Asante kocha,Imani yangu nimechagua kwa usahihi kukaa kwenye mchakato na kutekeleza mambo yote ninayofundishwa.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimeamua kukaa hapa na kufanya kwa vitendo. Nitafanya kadri mchakato unavyotaka. Nahitaji kuwa na mafanikio makubwa na Niko tayari kulipa gharama kuyapata.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimechagua kukaa hapa na kutekeleza kwa uhakika, ukubwa, bila hofu na bila sababu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Ujumbe huu mzito umenifikia, nimeusoma na nimeuelewa kikamilifu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ni utekelezaji tu na kukaa kwenye mchakato na kuonyesha ushaidi
Asante sana
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Makala hii imenishitua sana leo naahidi kuheshimu kila ambacho ni muhimu kwenye mchakato ambao tupo nao mpaka sasa..
LikeLike
Vizuri
LikeLike
MAARIFA + VITENDO = MAFANIKIO
Nimeamua kukaa hapa na kutekeleza kwa viwango vya juu sana, bila ya hofu wala sababu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Nipo hapa kwa ajili ya utekelezaji wa maarifa mbalimbali..
LikeLike
Safi.
LikeLike
Nimechagua kukaa kwenye mchakato na kutekeleza kwa vitendo maarifa ninayojofunza hapa.
LikeLike
Vizuri sana
LikeLike