3206; Raha ya ukuaji.
Rafiki yangu mpendwa,
Viumbe wote hai huwa wana sifa ya ukuaji.
Na sisi sote huwa tunafurahia sana ukuaji kwenye viumbe wote hai wanaotuzunguka.
Ukiwa na wanyama unaowafuga au mimea uliyopanda, ukuaji ndiyo kitu ambacho unakifuatilia sana.
Unakuwa unajua kila hatua ambapo kitu kipo na hatua gani inayofuata kwenye ukuaji.
Inapokuja kwenye watu muhimu kama watoto wetu, ufuatiliaji wetu kwenye ukuaji unakuwa ni wa karibu zaidi.
Wazazi ambao ndiyo kwa mara ya kwanza wanapata mtoto, huwa wanakuwa na shauku kubwa kwenye kila hatua ambayo mtoto anapiga.
Wakati mwingine wanahesabu kitu kuwa ukuaji wakati bado muda wake haujafika.
Kwa mfano mtoto ambaye bado ni mchanga kabisa, anapotoa sauti za ba ba ba.
Kwa matamanio makubwa ya ukuaji anbayo mzazi anakuwa nayo, anaweza kusema mtoto katamka baba.
Hata kama mtoto bado hajafikia kuongea, mzazi atafurahia hilo, japo siyo sahihi.
Nguvu hiyo ya ukuaji ipo kwenye kila eneo na kila kitu kwenye maisha yetu.
Inapokuja kwenye biashara tunazofanya, nazo zina nguvu ya ukuaji ndani yake.
Biashara zinazaliwa, kukua kisha kuzeeka na kufa.
Ili kuvuka kuzeeka na kufa, biashara inapaswa kubaki kwenye hatua ya ukuaji wa kasi mara zote.
Hapo ndipo raha ya ukuaji ilipo; unajua kabisa nini kinapaswa kutokea na una uwezo wa kusababisha matokeo hayo.
Wajibu wetu mkubwa kwenye biashara tulizonazo ni kuhakikisha mara zote zinakuwa kwenye ukuaji wa kasi.
Ni ukuaji huo wa kasi ndiyo unaiepusha biashara na changamoto mbalimbali zinazoweza kuiua.
Ukuaji wenyewe una hatari ya kuiua biashara, lakini hatari ni kubwa zaidi kama kusipokuwepo na ukuaji kabisa.
Hivyo una wajibu mkubwa wa kuhakikisha unaendelea kusukuma ukuaji kwenye biashara yako, kwa sababu ndipo nguvu ya kupona kwa biashara yako ilipo.
Ni raha iliyoje kuona kitu kinatoka hatua moja kwenda hatua nyingine, ambayo ni imara zaidi.
Hii ni raha ambayo una uwezo wa kuipata kila mara kupitia kuikuza biashara yako.
Una nafasi ya kuendelea kupata ushindi kupitia ukuaji endelevu wa biashara yako.
Chukua wajibu wako wa kuhakikisha biashara yako inaendelea kukua na upate raha kwa uendelevu.
Usiridhike na hatua yoyote ambayo biashara yako imefikia.
Bali jua kuna fursa ya kupiga hatua zaidi na zaidi.
Ni kupitia kuiwezesha biashara kupiga hatua hizo kwa msimamo ndiyo penye nguvu ya ukuaji endelevu wa biashara.
Kwenye biashara, unapoacha tu kukua, ndiyo unakuwa umeanza kuzeeka na kufa.
Zuia hatari hizo kwa kuiweka biashara yako kwenye mchakato wa ukuaji mara zote.
Mchakato huo utaiimarisha biashara na wewe mwenyewe pia.
Ufanyie kazi mara zote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwenye biashara unapoacha tu kukua, ndiyo unakuwa umeanza kuzeeka na kufa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana kocha. Ukuaji ni muhimu sana kwenye biashara. Nitaendelea kuweka mkazo ili biashara ikue zaidi
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Tufanyie kazi ukuaji ili boashara isizeeke na kufikia hatia yakurudi nyuma tuendelee kuiweka team kwenye hatua ya kukua siku hadi siku ili kuifurahia ukuaji wake kama mtoto anavyokua huku unamfurahia
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ni kweli kabisa ukuaji ni muhimu sana kwenye biashara na unaweza kukufanya wewe uweze kufikia lengo lako ulilojiwekea Ila kama hakuna ukuaji unashindwa kutatua changamoto za kibiashara
LikeLike
Kweli kabisa
LikeLike
Siku zote mtapambana kujisukuma ili kukua na kukuza biashara
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nitazuia hatari zote kwa kuiweka biashara yangu kwenye ukuaji wa mchakato wa mara zote.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala, nitaendelea kufuatilia ukuani kwa umakini wa biashara yangu,katu na kamwe sitaruhusu kuzeeka kwa biashara yangu.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nguvu ya kupona kwa biashara yangu,ili isizeeke na kufa ni mimi kuhakikisha mda wote nasukuma ukuaji wa biashara yangu.✍️
LikeLike
Ni kujisukuma kwenye ukuaji.
LikeLike
Asante sana Kocha.
Nitaikuza biashara ili niwe na furaha
Nitakuza kwa msimamo ili kuvuka kuzeeka ja kufa kwa biashara yangu
LikeLike
Vizuri sana
LikeLike
Ni kweli kabisa ukuaji unaleta raha kwa chochote unachofanya na kinyume chake ni huzuni. Asante sana kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kwenye Biashara unapoacha tu kukua, ndipo unapoanza kuzeeka na kufa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha ukurasa huu unanikumbusha usemi ambao ndugu yangu alukuwa na ni sisitiza akisema kwamba kwenye biashara hakuna kujiambia kwamba mtaji umeshimama umebaki katikati hapana, kwenye biashara kuna kusonga mbele ao kurudi nyuma akimaanisha usipo songa mbele maana yake unarudi nyuma. Hii nimeifurahia sana nitauzingatia ukuaji kwenye biashara yangu
LikeLike
Lazima tuendelee na ukuaji
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza bila ukuaji ni kuzeeka na hatimaye kufa kwa biashara.
LikeLike
Tuzingatie hilo.
LikeLike
Nimejifunza jambo moja kubwa kwa namna yeyote ile ni lazima ukubali kukua na ukubali kupiga hatua kubwa katika kile ambacho unafanya..
LikeLike
Hilo halikwepeki
LikeLike
Ukuaji ndio mpango mzima kwenye,biashara inapokuwa inaleta raja na unapata hamasa zaid ya kuikuza
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kwenye biashara, unapoacha kukua ndiyo unakuwa umeanza kuzeeka na kufa, Lakini fahamu kuwa Ukuaji wa biashara wenyewe una hatari ya kuiua biashara, lakini hatari ni kubwa zaidi kama kusipokuwepo na ukuaji kabisa.
Asante sana Kocha
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ukuaji wa biashara ni muhimu. Pasipo ukuaji biashara inakufa.
LikeLike
Hakika
LikeLike
ASANTE sana nitaendelea kuikuza zaidi biashara yangu
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Nitaiweka biashara yangu kwenye ukuaji wakati wote.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
UKUAJI ni Raha na muhimu Sana kwa biashara yoyote. Nitahakikisha napiga hatua kwa Kasi katika kuikuza biashar
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitahakikisha kila wakati biashara yangu ninaisukuma ktk ukuaji ili iendelee kuwa hai .
Asante Sana kocha
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike