💯KCM2324008; Usizurure.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumatatuYaMalengo
Mwanamafanikio,
Mwaka huu wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kuweka umakini wetu wote kwenye kitu kimoja mpaka kitupe matokeo makubwa.
Na tunaachilia breki kupitia kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kuweza kupiga hatua kubwa.

💯 Neno la leo;
Leo ikiwa ni #JumatatuYaMalengo tunaangalia jinsi ambavyo watu wamekuwa wanazurura hapa duniani na kusahaulika haraka baada ya kufa kwao.
Kuna watu wa aina mbili;
Aina ya kwanza ni wale ambao wakifariki habari yao inaishia hapo hapo.
Aina ya pili ni wale ambao wanaendelea kuishi hata baada ya kufariki.
Kinachotofautisha aina hizo mbili za watu ni malengo.
Wasio na malengo wanaishia kuzurura tu hapa duniani na hakuna makubwa wanayoyafanya.
Lakini wenye malengo wanajua nini wanapaswa kufanya na kwa njia hiyo wanajikuta wakikamilisha makubwa.
Kutokuwa na malengo inaweza kuonekana ni rahisi kuishi, kwa sababu huna kinachokusukuma, unaenda tu na kila kinachokujia. Lakini ni maisha ambayo hayaachi alama yoyote.
Kuwa na malengo inaweza kuonekana ni vigumu kuishi, kwa sababu unasukumwa kufanya mambo magumu. Lakini ni maisha yanayoacha alama kubwa.
Kuwa na malengo ambayo unajikumbusha kwa kuyaandika kila siku na kupambana kuyafikia.
Hiyo ndiyo njia ya kuachilia breki kwenye maisha yako kwa kuacha kuzurura na kuweza kuishi kwa ukamilifu.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu njia mbili za kulipa gharama kwenye maisha. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/06/3232
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku unayokwenda kushika hatamu ya maisha yako na kuifanya kuwa ya kipekee kabisa kwako.
Kocha.
💯