💯KCM2324011; Kuvurugwa.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#AlhamisiYaUbunifu
Mwanamafanikio,
Mwaka huu wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kuweka umakini wetu wote kwenye kitu kimoja mpaka kitupe matokeo makubwa.
Na tunaachilia breki kupitia kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kuweza kupiga hatua kubwa.

💯 Neno la leo; Kuvurugwa
Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaangalia jinsi ambavyo ubunifu huwa haueleweki mwanzoni.
Mambo mengi ambayo watu huwa wanafanya kila siku kwenye maisha yao ni kutokana na mazoea yao wenyewe au kuiga wengine wanavyofanya.
Watu huwa wanafanya kwa mazoea kwa sababu ndiyo yanayokubalika tayari.
Kwa kufanya hayo yaliyozoeleka kufanywa, unapata matokeo ambayo yamezoeleka kupatikana.
Na hiyo inakuwa ni breki kwako kuweza kufanya makubwa na kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.
Ili kwenda nje ya mazoea na kupata matokeo ya tofauti, lazima uwe tayari kujaribu vitu vipya na vya tofauti.
Hapo ndipo ubinifu unapoingia na kuwa njia ya kuachilia breki za mazoea.
Lakini hilo linakuja na changamoto zake.
Pale unapofanya kitu cha tofauti na ilivyozoeleka, utaonekana umevurugwa.
Watu watakuona kama umechanganyikiwa, kwa kuacha vilivyozoeleka na kufanya vipya.
Unachopaswa kuelewa ni kwamba kila kitu kipya huwa kinaonekana hakina maana mpaka pale kinapoleta matokeo makubwa na ya tofauti.
Hivyo usiache kuwa na ubunifu wa kujaribu vitu vipya na bora kila wakati.
Usijali sana wengine wanakuchukuliaje kwa sasa, wewe endelea kutoa thamani kubwa kupitia utofauti unaokuwa nao na matokeo ya mwisho yatakupa heshima kwa wote.
Kama hakuna watu ambao hawakuelewi, watu ambao wanakuona umevurugwa na kuchanganyikiwa, maana yake hakuna mapya na makubwa unayofanya.
Maana yake unafanya kwa mazoea na utaendelea kupata matokeo ya kawaida.
Kuwa na ngozi ngumu ya kutokujali watu wanakuchukuliaje na mara zote fanya vitu kwa ukubwa na ubora wa tofauti.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuwapa watu kile wanachotaka. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/09/3235
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku unayokwenda kushika hatamu ya maisha yako na kuifanya kuwa ya kipekee kabisa kwako.
Kocha.
💯