💯KCM2324012; Kuelewana.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#IjumaaYaMawasiliano

Mwanamafanikio,

Mwaka huu wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kuweka umakini wetu wote kwenye kitu kimoja mpaka kitupe matokeo makubwa.

Na tunaachilia breki kupitia kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kuweza kupiga hatua kubwa.



💯 Neno la leo; Kuelewana.

Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaangalia umuhimu wa kuelewana ili kupata kile unachokitaka.

Chochote ambacho unakitaka kwenye maisha yako, wanacho watu wengine.
Ili watu hao wawe tayari kukupa kile walichonacho, ni lazima kwanza muelewane.
Na njia kuu ya kuelewana ni kupitia mawasiliano sahihi.

Mawasiliano sahihi ni yale ambayo mtu anasikia kile ambacho mwingine anaeleza na pia kuzipata hisia ambazo mtu huyo anazo.

Kuna watu huwa unasema unawaelewa sana.
Hao siyo kwa sababu tu umesikia wanachoeleza, bali pia wanakufanya uwe na hisia fulani ndani yako.

Mawasiliano sahihi ni moja ya njia za kuachilia breki zinazokukwamisha kufanikiwa.
Kushindwa kuwafanya watu wakuelewe na wafanye kile unachotaka wafanye ni kikwazo kikubwa kwa mafanikio yako.

Kuwa na mawasiliano sahihi, ambapo unaeleweka siyo tu kwa kusikika bali pia kwa hisia ni kitu chenye nguvu ya kukupa kila unachotaka.

Unapowasilisha kwa wengine, toa maelezo yanayoeleweka na yachanganye na hisia ambazo zitamteka yule unayemwasilishia.
Hisia za upendo, matumaini na tamaa zina nguvu ya kuwasukuma watu kuchukua hatua.
Hizo ni hisia ambazo unaweza kuzichochea kwa watu.

Pia wengine wanapowasilisha kwako, fuatilia kwa umakini mkubwa na hakikisha unajenga hisia ndani yako zinazokusukuma kuchukua hatua unazopaswa kuchukua.

Hakikisha unaeleweka na wengine kwa kile unachotoa na unawaelewa wengine kwa kile unachopokea.
Hiyo ndiyo njia ya kuelewana ambayo inakakilisha mawasiliano ambayo yanaondoa breki kwenye mafanikio ya wengi.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu dawa ya uraibu na usumbufu. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/10/3236

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku unayokwenda kushika hatamu ya maisha yako na kuifanya kuwa ya kipekee kabisa kwako.

Kocha.
💯