💯KCM2324013; Vikwazo.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumatatuYaMalengo

Mwanamafanikio,

Mwaka huu wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kuweka umakini wetu wote kwenye kitu kimoja mpaka kitupe matokeo makubwa.

Na tunaachilia breki kupitia kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kuweza kupiga hatua kubwa.

Kuyaishi malengo yako, ijue na kuifuata KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO, piga 0752977170 sasa kupata kitabu.



💯 Neno la leo; Vikwazo.

Leo ikiwa ni #JumatatuYaMalengo tunaangalia sababu inayokupelekea uone vikwazo na hata kukata tamaa.

Kwenye maisha na safari ya kupata mafanikio makubwa unayokuwa unayataka, huwa kuna vikwazo mbalimbali.

Lakini vikwazo hivyo huwa havina nguvu ya kukukwamisha kama wewe mwenyewe hujavipa nguvu hiyo.

Na vikwazo vinakuwa na nguvu ya kukuzuia pale unapovipa nafasi.
Unapoviangalia na kuanza kuvifikiria, unavifanya viweze kukuzuia.

Unaviona vikwazo pale unapoyaondoa macho yako kwenye lengo lako kubwa.
Hivyo ndivyo vikwazo vinavyopata nguvu kwako kwa sababu unakuwa umeacha kuliangalia lengo kuu.

Kwa maana hiyo basi, njia ya uhakika ya kuvuka vikwazo ni muda wote kupelekea umakini wako wote kwenye malengo yako makubwa.

Kila mara yaangalie na kuyafikiria malengo makubwa uliyonayo.
Kila wakati jione ukiwa umeshayafikia malengo makubwa uliyonayo.

Kufanya hivyo kunaondoa nafasi ya vikwazo na wasiwasi kukuzuia kupata unachotaka.

Kukata tamaa ni kitu ambacho hakipaswi kuwepo kabisa kwenye mipango yako.
Ndiyo maana hupaswi kujihangaisha na vikwazo vyovyote, kwa sababu havikuhusu.
Hakuna chochote kitakachoweza kukuzuia pale kipaumbele cha kwanza kwenye maisha yako kinapokuwa malengo yako makuu.

Ni pale unapoondoa umakini wako kwenye malengo makuu ndiyo unaona mambo ya kukutisha na kukukatisha tamaa.
Mara zote tawaliwa na malengo yako makuu ili kusiwepo na kitu chochote kinachokuwa kikwazo kwako.

Kuwa na malengo makubwa unayoyafikiria na kuyafanyia kazi muda wote ni njia ya uhakika ya kuachilia breki ambazo zimekuwa kikwazo kwako kufanikiwa kwa muda mrefu.
Tawaliwa na malengo yako makubwa muda wote ili unyime vikwazo nafasi ya kukuzuia usifanikiwe.


💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuwatambua kwa matendo. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/13/3239

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku unayokwenda kushika hatamu ya maisha yako na kuifanya kuwa ya kipekee kabisa kwako.

Kocha.
💯