💯KCM2324020; Majibu.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumamosiYaUtulivu

Mwanamafanikio,

Mwaka huu wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kuweka umakini wetu wote kwenye kitu kimoja mpaka kitupe matokeo makubwa.

Na tunaachilia breki kupitia kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kuweza kupiga hatua kubwa.

Utajiri ni kitu kizuri na muhimu kwenye maisha, na huu ndiyo mtaala wake, upate sasa kwa mawasiliano; 0752977170



💯 Neno la leo; Majibu.

Leo ikiwa ni #JumamosiYaUtulivu tunaangalia mahali ambapo tunaweza kupata majibu ya maswali yetu yote.

Huwa wanasema maisha ni fumbo.
Kuna mambo mengi ambayo huwa tunakutana nayo kwenye maisha, ambapo tunakuwa hatuyaelewi wakati tunakutana nayo.
Lakini baadaye tunakuja kuyaelewa na kuona yakiwa na mchango mzuri, japo wakati yanatokea tuliona ni mabaya.

Mambo mengi mapya tunayokutana nayo kwenye maisha huwa yanatuacha tukiwa na maswali mengi kuliko majibu.
Na kwa kuwa watu huwa hatuwezi kutulia kama hatuna majibu ya kitu, huwa tunachukua maelezo yoyote tunayoweza kuyapata, hata kama siyo ya kweli.

Kila kitu kinachotokea kwenye maisha huwa kina maana.
Utaweza kujua maana ya kitu kama utajipa muda wa kukaa kwa utulivu na kutafakari kwa kina.
Kupitia ukimya na kutafakari, unaipa akili yako kazi ya kupitia kila kitu kwa kina na kuja na majibu sahihi.

Uzuri wa akili zetu binadamu zina mkusanyiko mkubwa wa mambo yote ambayo yamewahi kutokea kwenye maisha yako.
Mambo hayo yote yana majibu mengi ya yale unayokuwa unayapitia sasa kwenye maisha yako.

Popote ulipo sasa, ni wewe mwenyewe umejiweka hapo kwa kujua au kutokujua.
Kwa mambo uliyofanya au kushindwa kufanya huko nyuma yamekufikisha hapo ulipo sasa.
Ili kupata majibu sahihi ya jinsi ulivyofika hapo ulipo na namna bora ya kutoka hapo na kupiga hatua zaidi, tenga muda tulivu wa kutafakari kwa kina.

Usiendeshe maisha yako kwa mazoea au kufuata mkumbo. Badala yake pata majibu sahihi ya kila kitu ili uweze kuchukua hatua sahihi.

Hakuna kitu chochote kwenye maisha yako ambacho hakina majibu sahihi.
Tenga muda wa kuwa tulivu na kwenye muda huo tafakari jambo kwa kina ili kupata majibu sahihi.

Utulivu, kutafakari na kutahajudi ni moja ya njia za kuachilia breki za msongo wa mawazo ambazo watu wengi wanakwamishwa nazo.
Wewe usikubali kuwa kizuizi kwako mwenyewe, pata majibu sahihi ya maswali mbalimbali uliyonayo kwenye maisha ili uweze kuchukua hatua sahihi.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kufanya mara moja moja na kila mara. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/11/18/3244

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuweka picha kubwa ya mafanikio unayoyataka kwenye fikra zako.

Kocha.
💯