💯KCM2324033; Moja.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#IjumaaYaMawasiliano

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

0678977007



💯 Neno la leo; Moja.

Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaona jinsi ambavyo kwenye kila mawasiliano unapaswa kuwa na ujumbe mmoja mkuu unaotaka upande wa pili uuelewe ili mawasiliano yakamilike.

Moja ya sababu zinazopelekea mawasiliano mengi kuvunjika au kutokukamilika ni pale mtu anapojaribu kuwasilisha mambo mengi kwenye mawasiliano ambayo anafanya.
Hali hiyo inaishia kuwachanganya wale wanaolengwa na mawasiliano hayo.

Kuondokana na hilo unapaswa kuchagua ujumbe mmoja mkuu ambao kila mawasiliano unayofanya unawasilisha.
Kwa kuwa na ujumbe mmoja mkuu, sehemu kubwa ya mawasiliano inakuwa ni kufafanua zaidi na kuhakikisha upande wa pili umeelewa.

Ujumbe huo mkuu unapaswa kuelezewa kwa lugha rahisi ambayo mtu yeyote anaweza kuelewa na kuondoka na hatua anazopaswa kwenda kuchukua.

Watu wengi hupima mafanikio ya mawasiliano yao kwa wingi wa taarifa wanazokuwa wametoa.
Lakini hicho siyo kipimo sahihi, kwa sababu haijalishi umetoa taarifa nyingi kiasi gani, kama hujaeleweka, mawasiliano hayajakamilika.

Kipimo sahihi cha mafanikio ya mawasiliano ni kueleweka vizuri na watu kuweza kuchukua hatua ambazo zimedhamiriwa kwenye mawasiliano hayo.
Na njia pekee ya kufanikisha hilo ni kuwa na ujumbe mmoja mkuu ambao ndiyo kiini cha kila mafanikio unayoyafanya.
Ujumbe huo unarudiwa rudiwa na kufafanuliwa kwa kina kiasi kwamba hata kama mtu atasahau kila kitu, bado atabaki na ujumbe huo mkuu.

Tukianzia kwenye haya mawasiliano ninayofanya hapa na wewe, yatakuwa yamekamilika kama utaondoka hapa na ujumbe huu mkuu; kwenye kila mawasiliano unayofanya, chagua ujumbe mmoja mkuu wa mtu kuondoka nao.
Kabla hujafanya mawasiliano ya aina yoyote ile, jiulize kwanza nini lengo la mawasiliano hayo na upi ni ujumbe mkuu ambao upande wa pili unapaswa kuondoka nao.
Ukiweza kufanya hayo kwa usahihi, utakamilisha mawasiliano vizuri na kuweza kupata kile unachotaka.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kitakachokuondoa kwenye mchezo haraka zaidi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/01/3257

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kukamilisha mawasiliano kwa kuwa na ujumbe mkuu mmoja.

Kocha.
💯