💯KCM2324034; Upweke.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumamosiYaUtulivu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Ndani yako kuna nguvu kubwa sana ambayo ukiweza kuifikia na kuitumia utaweza kufanya makubwa sana. Tuwasiliane sasa kwa 0678977007



💯 Neno la leo; Upweke.

Leo ikiwa ni #JumamosiYaUtulivu tunaona jinsi ambavyo utulivu ndiyo njia ya kugundua huna upweke.

Tunaishi kwenye zama ambazo watu wengi wana upweke mkubwa.

Ni zama ambazo watu wamezungukwa na njia mbalimbali za kujumuika na wengine, lakini bado wanajikuta wakiwa kwenye upweke mkubwa.

Kinachofanya watu wawe na upweke mkubwa kwenye zama hizi ambazo fursa za kuchangamana na wengine ni nyingi ni hali ya kukosa utulivu.

Kadiri watu wanavyohangaika na mambo mengi na kukosa muda wa kuwa tulivu, wao na nafsi zao ndivyo wanavyojikuta wakiwa wapweke.

Njia pekee ya mtu kuondokana na upweke ni kujenga mahusiano mazuri na yeye binafsi.
Na mtu anaweza kufanya hilo kwa kutenga muda ambao anakuwa na utulivu mkubwa kwenye maisha yake.

Kwenye muda huo wa utulivu ndiyo anayatafakari maisha yake kwa kina na kuweza kujijua yeye mwenyewe vizuri.
Kwa mtu kujijua vizuri, anakuwa hana utagemezi mkubwa kwa wengine ili kujiona amekamilika.
Kwa mtu kujitosheleza mwenyewe hawezi kujiona mpweke.

Kila siku tenga muda kwa ajili yako mwenyewe, muda wa kuwa tulivu, kuwa na wewe mwenyewe.
Wewe mwenyewe ndiye mtu ambaye huwezi kujisaliti kwa namna yoyote ile.
Hivyo huwezi kuwa mpweke kama una mahusiano mazuri na wewe mwenyewe.

Kukosa utulivu ni breki ambayo imekuwa inawazuia wengi kufanya makubwa kwa kujiona ni wapweke. Upweke huo unawasukuma wahangaike na mengi yasiyo na tija ili tu kuwafurahisha wengine.
Wewe usiwe hivyo, jenga utulivu mkubwa kwenye maisha yako na imarisha mahusiano yako na wewe mwenyewe.
Hivyo ndivyo utakavyoweza kufanya makubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MTAALA WA UTAJIRI na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kufanya yale ambayo wengi hawafanyi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/02/3258

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kutenga muda tulivu wa kuwa na wewe mwenyewe ili kuondokana na upweke kwenye maisha yako.

Kocha.
💯