3271; Ahadi hewa.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu huwa wanatupa ahadi mbalimbali na sisi huwa tunaweka matumaini makubwa kwenye ahadi hizo.
Lakini unapofika muda wa watu hao kutekeleza ahadi walizoweka ndiyo tunagundua zilikuwa ni ahadi hewa tu.
Kadiri ahadi zinavyokuwa nyingi na nyingi zikawa hewa, ndivyo tunavyoumizwa kwa kutotimizwa kwa ahadi hizo.
Hilo huwa linaweza kupelekea mtu kukosa imani na ahadi zinazowekwa na wengine.
Lakini hilo siyo sahihi,
Pamoja na ahadi nyingi kuwa hewa, bado haifai kukosa imani kwenye ahadi zote kabisa.
Ili kujua ipi ahadi sahihi na ipi hewa, kuna viashiria vya wazi huwa vinakuwepo. Ukishaviona viashirikia hivyo, unakuwa unajua dhahiri kama ahadi ni hewa au ya uhakika.
Moja ni jumla na maalumu.
Watu wanaoahidi mambo ya jumla huwa wanatoa ahadi hewa. Na wale wanaoahidi mambo maalumu huwa zinakuwa ni ahadi sahihi.
Kwa mfano mtu anapokuambia; “Nitafute pale unapohitaji chochote” huwa inakuwa ni ahadi hewa tu ya kuachana na wewe.
Lakini pale ahadi inapokuwa maalumu, mfano; “Nitafute pale unapohitaji msaada kwenye …. ” ni ahadi inayokuwa halisi zaidi.
Mbili ni urahisi na uharaka wa kuahidi.
Pale mtu anapokuahidi kwa urahisi na haraka, jua wazi hiyo ni huduma hewa. Mtu anakuwa amefanya hivyo ili tu kumalizana na wewe.
Ahadi yoyote ambayo inatoka haraka na kwa urahisi, ni ahadi ya kuwa na wasiwasi nayo.
Ahadi halisi inamchukua mtu muda wa kutafakari kwa kina na kuangalia uhakika wake wa kutekeleza kabla ya kuitoa.
Unapopewa ahadi kwa haraka na urahisi, usiweke imani kubwa kwenye ahadi hizo. Kufikiri hivyo kufakuepusha na hali za kukatishwa tamaa na ahadi hewa zinazowekaa na wengine.
Tatu ni hisia wakati wa ahadi.
Ahadi yoyote inayotolewa wakati mtu ana hisia kali, iwe ni chanya au hasi, huwa inaishia kuwa ahadi hewa.
Mtu anayeahidi akiwa kwenye hali ya furaha sana au huzuni sana hawezi kutoa ahadi sahihi na za kweli.
Pale hisia za mtu zinapokuwa juu, fikra huwa zinashuka na hapo mambo mengi kuwa siyo sahihi.
Unapogundua mtu yupo kwenye hisia kali, anapokupa ahadi ya chochote, mtafute tena akiwa kwenye akili yake timamu kabla hujaweka mategemeo makubwa kwenye anadi hizo.
Watu wengi wanaokupa ahadi, hawazimaanishi ahadi zao.
Wengi wanatumia ahadi kama sehemu ya kukutoroka.
Kwa kujua changamoto hii iliyopo kwenye ahadi, hakikisha unajijengea mfumo mzuri kwako binafsi kwenye kuchuma ahadi unazopokea.
Kwa kuweza kuzitambua ahadi hewa na kuachana nazo, inakupa muda na umakini wa kufuatilia ahadi sahihi kwako.
Usiwalaumu tena watu pale wanapokuahidi halafu wasitekeleze.
Unapoweka matarajio makubwa kwenye ahadi za wengine, unajiweka kwenye nafasi ya kuanguka na kushindwa.
Chuja vizuri ahadi unazopewa na wengine ili uweze kufuatilia kwa usahihi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kila ahadi inapaswa kupimwa uhalisia wake wakati inatolewa ili isije ikakuhadaa na kukupotezea muda.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Kumbe ni muhimu kuchuja kwa makini ahadi unazopewa ili tusiziweke kwenye matumaini kumbe ni ahadi hewa
Asiwe na hisia
Afikirie wakati wa kutoa ahadi
Wakati wa kutoa ahadi isiwe ya jumlajumla
LikeLike
Ndiyo, tuwe makini sana na ahadi tunazopewa.
LikeLike
Unapoweka matarajio makubwa kwenye ahadi za wengine, unajiweka kwenye nafasi ya kuanguka na kushindwa.
LikeLike
Ndiyo, ni vyema kuwa na matarajio madogo.
LikeLike
Tuagalie ahadi tunazopewa tuzichinguze na kuzifanyia kazi kama ni hewa au zenye maana
Asante
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitazingatia jumla na ma alum, uharaka na hisia wakati mtu anatoa ananipa ahadi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Pale hisia za mtu zinapokuwa juu, fikra huwa zinashuka na hapo mambo mengi kuwa siyo sahihi.✍️
LikeLike
Kabisa
LikeLike