💯KCM2324048; Maongezi.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumamosiYaUtulivu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Kujifunza kwa kina zaidi jinsi ya kupata utulivu kupitia kufanya tahajudi, pata kitabu hiki. Mawasiliano; 0678 977 007



💯 Neno la leo; Maongezi.

Leo ikiwa ni #JumamosiYaUtulivu tunaona jinsi ambavyo utulivu unavyotoa fursa ya maongezi yako na nafsi yako.

Kwenye hali ya maisha ya kawaida huwa tunakuwa na usumbufu mwingi na unaotawanya umakini wetu.

Ni kwenye usumbufu huo ndiyo tunajikuta tukihangaika na mambo mengi yasiyokuwa na tija huku tukiyasahau yale yenye tija zaidi.

Moja ya mambo yenye tija tunayoyasahau ni maongezi na nafsi zetu wenyewe.
Nafsi zetu zinajua mengi kuhusu sisi, lakini zimekuwa hazipati nafasi ya kutoa hayo mengi kwa sababu hatuzisikilizi.

Ili kusikiliza nafsi yako, lazima utenge muda tulivu ambao utakuwa peke yako. Kwenye muda huo unaepuka usumbufu wa kila aina kwa kuwa eneo tulivu na kuisikiliza nafsi yako.

Kwa kuwa na utulivu na kufanya maongezi na nafsi yako utapata mengi ambayo yatakusaidia sana kufanya maamuzi sahihi na yenye tija kwako.

Watu wengi wanalazimika kuiga wengine na kufuata mkumbo kwa sababu hawajui nini wanapaswa kufanya. Na wanakuwa hawajui nini wanapaswa kufanya kwa sababu hawajawahi kufanya maongezi na nafsi zao wenyewe.

Kukosa utulivu wa kukuwezesha kuisikiliza nafsi yako ni moja ya breki ambazo zimekuzuia kwa muda mrefu usipate unachotaka.
Sasa ni wakati wa kuachilia breki hizo, kwa kupanga kabisa muda wa kuwa tulivu na kufanya maongezi na nafsi yako.
Jipe miadi wewe mwenyewe kama unavyowapa wengine miadi.
Jitengee muda kwa ajili yako mwenyewe kama unavyowatengea wengine muda.

Maongezi yako na nafsi yako yanakupa fursa ya kujijua vizuri wewe mwenyewe na kujua kipi sahihi kufanya.
Kwa kujijua vizuri wewe mwenyewe utaweza kufanya maamuzi bora kabisa kwenye maisha yako.

Yote hayo yanaanza na wewe na utayari wako wa kufanya maongezi na nafsi yako. Usipuuze hili, ni muhimu sana.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu bora na sahihi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/16/3272

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kupata utulivu wa kufanya maongezi na nafsi yako ili kuweza kufanya maamuzi bora na kupiga hatua.

Kocha.
💯