3275; Wasioweza kuishi bila wewe.
Rafiki yangu mpendwa,
Safari ya mafanikio imekuwa ngumu sana kwa wengi kwa sababu wanapoteza rasilimali zao kwenye mambo yasiyokuwa na tija.
Unakuta mtu anakazana kumfikia kila mtu na kukubalika na watu wote.
Siyo tu kwamba hilo linakuwa haliwezekani, bali pia linawapoteza hata wale wazuri ambao wangefaa.
Kwa mtu kuhangaika kuwafikia wengi, anawapoteza wale wachache ambao wangefaa zaidi.
Kama unataka kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako, kazi yako siyo kumridhisha kila mtu.
Kazi yako kuu ni kuwatafuta watu ambao hawawezi kuishi bila wewe.
Hawa ni watu ambao wana uhitaji mkubwa wa kile unachofanya na maisha yao yanakitegemea sana.
Katika kuwapata watu hawa, kuna maswali matatu ambayo kila mtu anapaswa kuyajibu kwa usahihi ili kujua cha kufanyia kazi na kufanikiwa.
Swali la kwanza ni watu hao ni kina nani?
Watu ambao hawawezi kuishi bila wewe, yaani wanaotegemea kile unachofanya huwa wana sifa fulani za tofauti.
Zijue sifa kuu kwa upande wa kile unachofanya ili uweze kujua njia bora za kuwafikia.
Swali la pili ni vitu gani hasa ambavyo watu hao wanakuwa wanataka?
Matakwa huwa ndiyo yenye msukumo mkubwa wa kuwafanya watu wachukue hatua.
Ni muhimu kuyajua matakwa ya wale uliowachagua ili uweze kuwahudumia vizuri na kuwafanya kuwa tegemezi kwako.
Hakikisha unawapa kwa uhakika kile wanachotaka kiasi cha kuwafanya wakutegemee wewe kwenye hicho.
Na ukishakuwa wa kutegemewa, hamikikisha huvunji uaminifu huo.
Swali la tatu ni unawafikiaje watu hao?
Hili ni swali ambalo wengi huwa hawajiulizi kwa kuona majibu yake ni rahisi. Lakini siyo rahisi kama wengi wanavyodhani.
Ili majibu ya swali hili la tatu yawe sahihi, majibu ya swali la kwanza yanapaswa kuwa sahihi.
Ni lazima kwanza kuwajua watu sahihi kabla ya kujua ni wapi unapoweza kuwapata watu hao.
Kwa chochote kile unachofanya, jiulize na jipe majibu sahihi kwenye maswali hayo natatu kisha weka kwenye matendo hayo majibu yako.
Kwa kufanya hivi utaweza kutengeneza wateja maalumu kwako, ambao hawawezi kuishi bila ya wewe. Hapo ndipo ukuaji mkubwa na wa uhakika unaweza kufanyika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kuwajua kisha kujua unawapata wapi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kazi yangu si kumridhisha kila mtu.Ni kutafuta wale ambao hawawezi kuishi bila mimi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Mafanikio makubwa yanahitaji kuishi bila kumridhisha kila mtu.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni kweli na hili litawezekana tu pale utakapoaafikia wengi na kuwachambuaa ili upate sasa hao ambaowatakutegemea lakini pia uwe unawahudumia kwa wakati na wao wakutegemee
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Huwezi kuwafikia watu wote Bali kujua -:
Nani,?
Nini wanataka?
Unawapataje?
Weka nguvu kupata majibu hayo matatu.
🙏🙏🙏
LikeLike
Hakika
LikeLike
Wajue watu wape kile wanataka na hapo utatengeneza watu wasioweza kuishi bila wewe
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
LikeLike
👏
LikeLike
Asante sana kocha, kutafuta watu ambao hawawezi kuishi bila Mimi ili kuwapa mahitaji yao sahihi
LikeLike
Karibu
LikeLike
Natengeneza jamii ya wateja ambao hawawezi kuishi bila Mimi Ili nipate mafanikio makubwa, kwanza niwajue ni kina nani, matakwa yao na wapi wanapatikana Kisha kuweka kwenye matendo.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Watu Hao ni kina nani,. Vitu wanavyotaka na nawafikiaje watu hao.
LikeLike
Ni muhimu kujua.
LikeLike