💯KCM2324050; Muhimu.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumanneYaKujikubali
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.
💯 Neno la leo; Muhimu.
Leo ikiwa ni #JumanneYaKujikubali tunaona jinsi ambavyo wewe una umuhimu mkubwa kwa wengine.
Ni rahisi kujichukulia kawaida hasa pale unapokuwa umeshazoea kile unachofanya.
Lakini ukweli ni kwamba wewe ni wa muhimu sana kwa baadhi ya watu wanaotegemea kile unachofanya.
Kuna watu ambao wanaweka mipango yao muhimu kwenye maisha kwa kutegemea kile unachofanya wewe, hata kama unakiona ni cha kawaida kiasi gani.
Lakini pia kuna watu ambao bado hujakutana nao na maisha yao hayajawa bora kama wanavyotaka. Ni mpaka pale watakapokutana na wewe ndiyo maisha yao yatabadilika kabisa.
Hivyo una umuhimu mkubwa sana mpaka kwa watu ambao bado hujajuana nao.
Kwa kila mtu unayekutana naye, kuna kitu cha tofauti unasababisha kwao. Kuna alama fulani ambayo unaiacha kwenye maisha yao ambayo haitafutika kamwe.
Muhimu ni wewe kujua ni eneo gani ambalo unaweza kuacha alama hiyo kwa watu na kulifanyia kazi kwa uhakika.
Huwa wanasema ukitaka kujua hakuna kisichokuwa na madhara, jaribu kulala kwenye chumba ambacho kina mbu hata mmoja tu. Kwa hakika mbu mmoja anaweza kuvuruga usingizi wako wote.
Usijichukulie poa wala kujidharau.
Jikubali na kujiheshimu.
Jua una umuhimu mkubwa sana kwa baadhi ya watu kwenye hicho unachofanya.
Waridhishe vyema watu hao ambao una umuhimu mkubwa kwao na utaweza kufanya makubwa sana.
Kutokujikubali ni breki ambayo imewakwamisha wengi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Achilia kabisa breki hii kwa kujikubali sana wewe mwenyewe.
Na hujikubali kwa kujifariji, bali kwa kuwaangalia wale wanaonufaika sana na kile unachofanya.
Kwa kuona jinsi unavyoyagusa maisha ya wengine, utaona jinsi ulivyo muhimu na hivyo kuweza kujikubali.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu wasioweza kuishi bila wewe. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/19/3275
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kutambua umuhimu mkubwa ulionao kwa wengine na kujikubali ili uweze kuwanufaisha wengi zaidi.
Kocha.
💯