💯KCM2324057; Ukomo.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumatatuYaMalengo

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Ili utimize ndoto zako, unapaswa kuiishi kila siku kwa mafanikio. Pata kitabu hiki cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO uweze kutimiza hilo. Tuwasiliane; 0678 977 007



💯 Neno la leo; Ukomo.

Leo ikiwa ni #JumatatuYaMalengo tunaona jinsi ambavyo malengo ni ndoto zenye tarehe ya ukomo.

Kila mtu kwenye maisha huwa ana ndoto mbalimbali, kubwa na ndogo.
Kuota ni bure kabisa.
Tangu tukiwa watoto tumekuwa tunapata picha kubwa ya nini hasa tunachotaka kwenye maisha.

Lakini ili ndoto tulizonazo ziweze kuwa uhalisia, tunapaswa kuziwekea tarehe ya ukomo.
Kwamba ni lini hasa tunataka kile ambacho ni ndoto kwetu kiwe kwenye maisha yetu halisi.
Hapo ndipo ndoto zinapogeuka na kuwa malengo.
Ukishaziwekea ndoto tarehe ya ukomo, zinaacha kuwa ndoto na badala yake kuwa malengo.

Malengo ni ndoto ambazo zinafanyiwa kazi kwa uhakika ili kuweza kufikia kwenye kipindi fulani.
Bila ya ukomo wa muda, malengo hayawezi kuwa malengo, bali yanabaki kuwa ndoto.

Ni tarehe ya ukomo ndiyo inamsukuma mtu kuchukua hatua kutimiza kitu.
Hasa pale tarehe hiyo ya ukomo haiwezi kuahirishwa au kusogezwa mbele.

Kama una ndoto ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu lakini huzifikii, hebu anza kwa kuziwekea tarehe ya ukomo.
Weka tarehe ya ukomo ambayo itakuwa na madhara kwako kama hautaitimiza.
Na hilo litakusukuma kuchukua hatua kubwa ili uweze kuzifikia ndoto hizo.

Madhara unayoweza kujiwekea kwenue tarehe ya ukomo kwenye ndoto zako ni kuwahusisha wengine ambao watakuwajibisha pale utakaposhindwa kwenye hiyo tarehe uliyojipangia.

Peke yetu ni rahisi sana kujidanganya.
Kama kweli tunataka kuzifikia ndoto kubwa tulizonazo, tunapaswa kuzigeuza kuwa malengo.
Kwa kuweka kabisa hatua za kuchukua na tarehe ya mwisho ya kufikia.
Kisha kuwepo na madhara kama hatutaweza kutekeleza hivyo.

Hilo litaondoa breki ya kukosa malengo ambayo imekuwa kikwazo kwa wengi kufanikiwa licha ya kuwa na ndoto kubwa.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu uhakika wa ushindi. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/25/3281

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuweka tarehe ya ukomo kwenye ndoto zako ili yawe malengo unayoyafanyia kazi.

Kocha.
💯