💯KCM2324060; Kujishtukia.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#AlhamisiYaUbunifu

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Kuwa na kanuni unayoitumia kuendesha kila siku yako kunaibua ubunifu mkubwa ndani yako. Pata kitabu sasa; 0678 977 007



💯 Neno la leo; Kujishtukia.

Leo ikiwa ni #AlhamisiYaUbunifu tunaona jinsi ambavyo kujishtukia ni adui mkubwa wa ubunifu.

Ubunifu ni kwenda kinyume na mazoea ambayo yapo, kupingana na kundi kubwa la watu.
Hicho ni kitu ambacho kinahitaji ujasiri mkubwa sana kufanya.

Wengi kutokuwa wabunifu siyo kwa sababu hawana ubunifu ndani yao, bali kwa sababu ya kujishtukia au kutokujiamini vya kutosha kwenye kile wanachoona ni tofauti.

Watoto wadogo huwa wanaonekana ni wabunifu sana, hiyo ni kwa sababu huwa hawajishtukii sana kama watu wazima. Wakiwaza kitu wanakiropoka kama kilivyo, hawajiulizi kama watakubalika na wengine au la.

Hadithi ya mfalme aliye uchi inadhihirisha hilo. Watu wazima wote waliona mfalme yupo uchi, lakini kwa kuwa wengi walisema amevaa nguo, nao walienda na huo mkumbo.
Ni mpala pale mtoto alipouliza mbona mfalme yupo uchi? Hapo ndipo wengine nao wakafunguka.

Labda nikuulize wewe, ni mara ngapi umepata wazo la kufanya kitu kwa namna fulani ya tofauti, lakini kwa sababu wengine wote wanafanya kwa namna fulani ukaona hiyo ndiyo sahihi zaidi. Halafu baadaye ukaja kukutana na ambaye anafanya kwa ile namna ya tofauti uliyowaza na anapata matokeo mazuri sana.

Ukiacha kujishtukia na kuanza kujiamini kwenye kila unachofikiri na kukifanya, utaonekana kuwa mtu mwenye ubunifu sana na kuweza kufanya makubwa.
Siyo kwamba utakuwa umewazidi wengine kwenye ubunifu, bali ni ile kujiamini kuliko wao ndiyo inakuwa imekusaidia.

Kwenye mambo yaliyo mengi, majibu ya kipi sahihi kufanya huwa tunayo tayari. Kinachotukwamisha ni kujishtukia, hasa pale wengi wanapokuwa wanafanya tofauti na tunavyotaka kufanya sisi.

Rudi utotoni, kwa kila wazo la tofauti unalokuwa nalo usilizike kwa sababu tu wengi wanafanya tofauti na wazo hilo.
Badala yake tekeleza hayo mawazo ya tofauti unayokuwa nayo kwenye kuboresha kile unachofanya.
Ni kwa njia hiyo ndiyo utaweza kuzalisha matokeo makubwa na ya tofauti kabisa.

Jikubali, jiamini na tekeleza kile tofauti unachofikiria bila ya kujali wengine wanafanya nini sasa.
Wengi tayari wana mawazo ya tofauti kama wewe, ila tu hawana ujasiri wa kuyatekeleza.
Anza wewe kuyatekeleza mawazo hayo ya tofauti na utapata wafuasi wengi, hasa pale utakapoweza kuzalisha matokeo bora zaidi ya ilivyozoeleka.

Usiogope kushindwa kwa kujaribu vitu vipya, bali ogopa kushindwa kwa kufuata mkumbo na kufanya kwa mazoea.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuanza na kumaliza. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/12/28/3284

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuacha kujishtukia na kutekeleza mawazo ya kibunifu unayoyapata ili kupata matokeo bora.

Kocha.
💯