💯KCM2324065; Ubinafsi.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumanneYaKujikubali

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

0678 977 007 kupata kitabu



💯 Neno la leo; Ubinafsi.

Leo ikiwa ni #JumanneYaKujikubali tunaona jinsi ambavyo kujikubali na kujijali siyo ubinafsi, bali ni usimamizi mzuri wa zawadi pekee uliyopewa.

Tumejengewa hali ya kuwajali wengine kabla yetu wenyewe na kuona hilo ndiyo sahihi.
Ni kitu kizuri kuwajali wengine, lakini kama utafanya hivyo bila ya kujijali wewe mwenyewe, inakuwa haina maana kabisa.

Kuna zawadi kubwa sana ambayo ipo ndani yako kwa ajili ya dunia.
Zawadi hiyo imewekwa ndani yako, lakini manufaa yake ni kwa dunia nzima.
Njia pekee ya kutumia zawadi hiyo na ikawa na manufaa kwa wengine ni kujikubali na kujijali.

Ni kupitia kujikubali na kujijali ndiyo unaweza kusimamia vizuri zawadi kubwa iliyopo ndani yako na ikawa na manufaa kwa dunia nzima.

Usikubali kujiona una hatia pale unapojikubali na kujijali wewe mwenyewe kwanza kabla ya wengine.
Hiyo ni hatua muhimu ya kuweza kutoa zawadi yako kwa ajili ya wengine.

Kutokujikubali na kutokujijali kwa kisingizio cha kutokuwa mbinafsi ni kujiwekea breki kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Achilia breki hiyo ambayo imekuwa inakuzuia kwa muda mrefu.
Kubali kwamba kujikubali na kujijali ni hatua muhimu ya kuweza kuwanufaisha wengine zaidi.

Utafanya mengi makubwa kwa kufanya yale yanayochukuliwa ni ubinafsi, kuliko unavyoweza kufanya kwa kutaka kuonekana unajali zaidi.
Ubinafsi sahihi una manufaa makubwa kwako na hata kwa wengine pia.
Usikubali kuondolewa kwenye hali ya kujikubali na kujijali, hiyo ndiyo yenye msukumo kwako kufanya makubwa zaidi.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kusubiri kuanza. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/02/3289

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kujikubali na kujijali ili kuweza kuitoa zawadi iliyopo ndani yako kwa manufaa ya wengine.

Kocha.
💯