💯KCM2324066; Kuonewa.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumatanoYaUwajibikaji

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

Fikia na tumia uwezo mkubwa ulio ndani yako kujenga mafanikio makubwa. 0678 977 007



💯 Neno la leo; Kuonewa.

Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo kuwa na mtazamo wa kuonewa kunapunguza uwezo mkubwa wa mtu kufanya makubwa.

Mtazamo wa kuonewa au kuathirika imekuwa sehemu ambayo wengi wanajificha.
Pale wanaposhindwa kupata wanachotaka, wanatafuta watu wa kuwalaumu na kuwalalamikia.

Kinachotokea ni pale watu wanapokuwa na mtazamo wa kuonewa au kuathirika, wanapunguza ule uwezo mkubwa ulio ndani yao ambao ungewawezesha kufanya makubwa.

Kila binadamu tayari anao uwezo mkubwa ndani yake.
Uwezo ambao ungemwezesha kukabiliana na kila aina ya kitu anachokutana nacho kwenye maisha.
Lakini mtu hawezi kufikia uwezo huo kama hatachukua uwajibikaji juu ya maisha yake mwenyewe.

Ni kwa kukubali kuwajibika kwenye kila eneo la maisha yako ndiyo unaweza kuyaboresha maisha yako na kufanya makubwa sana.
Hilo haliwezi kwenda pamoja na hali ya mtu kuona unaonewa.

Haijalishi nini kimetokea kwenye maisha yako na nani aliyekisababisha, wewe ndiye unayewajibika.
Kutambua uwajibikaji wako mapema kutakusaidia uweze kuvuka mengi mapema na kupata matokeo mazuri.

Kulalamika, kulaumu, kuona unaonewa na kujichukulia kama mwathirika ni breki kubwa sana inayowazuia wengi kupiga hatua kubwa kwenye maisha yao.
Wewe achilia kabisa breki hizo zote kwa kuwa na uwajibikaji mkubwa kwenye kila eneo la maisha yako.

Wajibika kwa kila kitu kwenye maisha yako na utaweza kutumia uwezo mkubwa uliopo ndani yako kufanya makubwa zaidi.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu unachoshindana nacho. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/03/3290

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuweza kufanya makubwa kwa kukubali uwajibikaji kamili wa maisha yako na kukataa kuona unaonewa au ni mwathirika.

Kocha.
💯