💯KCM2324069; Chanzo.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumamosiYaUtulivu
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Chanzo.
Leo ikiwa ni #JumamosiYaUtulivu tunaona jinsi ambavyo kukosa utulivu ndiyo chanzo kikuu cha matatizo yote ambayo mtu anakuwa nayo.
Vitu vingi kwenye maisha havihitaji wewe uchukue hatua yoyote ile.
Ni subira na utulivu wako ndiyo vinakuwa vinahitajika zaidi ili mtu kuweza kufanya makubwa.
Kwenye utulivu ndiyo mtu anaweza kutafakari kwa kina kuhusu kitu na kujua hatua sahihi za kuchukua.
Kupitia utulivu mtu anaepuka kuchukua hatua ambazo zina madhara makubwa zaidi.
Wakati wa kukabiliana na changamoto mbalimbali ndiyo pia huwa wakati ambao matatizo mengi zaidi.
Utulivu mkubwa unahitajika sana ili kuepuka hayo matatizo.
Ni muhimu sana mtu kuhakikisha unapata muda tulivu wa kuyatafakari maisha yako kila siku.
Kwa sababu ni ndani ya muda huo ndiyo mtu unaweza kupata majibu sahihi ya mambo mengi unayopitia.
Kwa bahati mbaya sana, watu wengi hawana ujuzi wa kukaa kwenye utulivu kwa muda mrefu.
Watu wameshazoea usumbufu kiasi kwamba hata wakiwa peke yao, lazima watafute kitu cha kuwasisimua.
Kutatua matatizo tuliyonayo na kuepuka kutengeneza matatizo mengine mapya, tuhakikishe tunatenga muda wa kuwa na utulivu na kuutumia kutafakari kwa kina yale tunayopitia na kujipa majibu sahihi ya hatua za kuchukua.
Kukosa utulivu ni breki inayowazuia wengi kupiga hatua kubwa.
Achilia breki hiyo kwa kujijengea utulivu kwenye maisha yako.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu kuepuka kifo. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/06/3293
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kupata utulivu ili kuweza kutatua na kuepuka matatizo mbalimbali ya maisha.
Kocha.
💯