Kila mtu anataka mafanikio makubwa kwenye maisha yake. Lakini kiuhalisia ni watu wachache sana ambao huwa wanayapata mafanikio makubwa wanayoyataka.
Licha ya mafunzo mengi ya mafanikio kutolewa, ambayo yanaeleza yale ya msingi kwa watu kuzingatia ili kufanikiwa, bado wengi wamekuwa hawapati mafanikio makubwa.
Hiyo ni kwa sababu kuna ukweli ambao umekuwa hauwekwi wazi kuhusu mafanikio. Na siyo kwa sababu ukweli huo siyo sahihi, bali kwa sababu ukweli huo unaumiza na watu wengi huwa hawapendi kuumia.

Watu wengi huwa wanapenda kusikia vitu vinavyowafurahisha na hivyo mara zote kutafuta kusikia vitu vya aina hiyo. Wanaposikia vitu ambavyo haviwafurahishi, hata kama ni kweli, huwa hawapendezwi navyo na hivyo kuanza kuwashambulia wale wanaovisema.
Hilo limewafunza somo kubwa wote ambao wamefanikiwa. Kwa kutokuwa tayari kuhangaika na maelezo mengi kwa watu wasiotaka kusikia ukweli mchungu, wamekuwa wanasema yale watu wanapenda kusikia na kuacha yale ambayo watu hawapendi kusikia.
Njia rahisi ya kujua ukweli usiosemwa kuhusu mafanikio siyo kusikiliza kile ambacho waliofanikiwa wanasema, bali kuangalia kile walichokuwa wanafanya kabla ya kufanikiwa. Kwa sababu wanachofanya watu wakafanikiwa siyo wanachokuja kusema kimewapa mafanikio.
Na hili halimaanishi kwamba wanafanya uhalifu au mambo mabaya, bali ni ule ugumu na mateso ya safari nzima, ambayo imejaa maumivu makali ndiyo kitu ambacho wanakwepa kuwaambia wengine ambao hawapo tayari kupokea ukweli huo.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha baadhi ya kweli za mafanikio ambazo huwezi kuzisikia popote. Nimezieleza kwa mifano rahisi kabisa kwako kuelewa na japo zinaumiza, ukizikubali na kuziishi basi utaweza kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Karibu ujifunze kweli hizo kwa kusikiliza kipindi hicho hapo chini, ukachukue hatua na uweze kuyaboresha maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.