Watu wengi wanaodhani wanafanya uwekezaji, siyo wawekezaji hasa, bali ni wachuuzi wa uwekezaji. Hawa ni wale ambao wanafanya uwekezaji wakati bei ni ndogo, kisha bei inapoongezeka wanauza uwekezaji huo ili kupata faida.

Kinadharia, hilo la kununua uwekezaji kwa bei chini na kuuza kwa bei juu linaonekana kuwa na manufaa. Lakini kiuhalisia ni zoezi ambalo halina faida kabisa. Wengi wanaochuuza uwekezaji, huwa wanaishia kupata hasara.

Njia bora ya kunufaika na uwekezaji wowote unaofanya ni kwa kuwekeza na kukaa kitako. Hii ina maana kwamba ukishafanya uwekezaji, unakaa na kusubiri. Huhangaiki kuuza uwekezaji wako ili kupata faida ya haraka, badala yake unaupa uwekezaji wako muda wa kukua.

Manufaa makubwa ya uwekezaji huwa yanapatikana kwa kuuacha muda ufanye kazi yake. Ukishawekeza, huhitaji kufanya kitu kingine chochote zaidi ya kusubiri. Na hili ndiyo jambo gumu zaidi kwa walio wengi, kwa sababu huwa hawajisikii vizuri kukaa bila kufanya kitu. Msukumo wa kutaka kufanya vitu umekuwa chanzo cha hasara kwa walio wengi.

Unapowekeza, thamani huwa inakua kadiri muda unavyokwenda. Na kadiri muda unavyokuwa mrefu bila ya uwekezaji kuingiliwa, ndivyo manufaa yake yanavyokuwa makubwa zaidi.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza vizuri dhana hii ya uwekezaji wa kukaa kitako na jinsi unavyopaswa kuufanyia kazi. Kwa kuwa uwekezaji ndiyo njia kuu ya kutunza utajiri ambao mtu ameujenga kwenye kipato, unapaswa kuielewa dhana hii vyema.

Karibu usikilize kipindi hiki cha ONGEA NA KOCHA ujifunze na kuchukua hatua ili uweze kufanya uwekezaji sahihi na kujenga utajiri mkubwa. Kipindi kipo hapo chini.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.