💯KCM2324072; Wanavyokuchukulia.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#JumanneYaKujikubali
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Wanavyokuchukulia.
Leo ikiwa ni #JumanneYaKujikubali tunaona jinsi ambavyo kujali wengine wanavyotuchukulia ni kushindwa kujiamini wenyewe.
Vile ulivyo, tayari una kila unachohitaji ili kupata kile unachotaka.
Lakini umekuwa hupati unachotaka kwa sababu unajali sana wengine wanavyokuchukulia.
Unapopanga ufanyaji wako wa mambo kwa kuzingatia jinsi ambavyo wengine wanakuchukulia, hutaweza kufanya chochote ambacho ni kikubwa.
Kwani utajikuta unafanya zaidi yale yanayowafurahisha wengine.
Kwa bahati mbaya sana, yanayowafurahisha wengine siyo yanayokupa matokeo unayotaka.
Hivyo hilo linamweka mtu njia panda, afanye kile anachotaka au kinachokubalika na wengine?
Wengi, kwa kupenda kumridhisha kila mtu huwa wanajikuta wameingia kwenye mtego wa kufanya yale yanayowaridhisha wengine.
Ubaya wa kufanya mambo ili kuwaridhisha wengine ni watu huwa hawaridhiki, hasa kwa mambo ya nje.
Hivyo hata uhangaike kiasi gani kuwaridhisha, bado wataendelea kutaka zaidi kutoka kwako.
Na kadiri unavyoendelea kutaka kuwaridhisha, ndivyo unavyozidi kupotea kwenye yale hasa unayoyataka.
Jiamini, jikubali na jiridhishe wewe mwenyewe.
Kwani hata usiporidhika na yale unayopata, msukumo wako wa ndani wa kufanya zaidi utakuwezesha kupiga hatua kubwa.
Wengine watakuchukulia vile wanavyotaka wao wenyewe, hakuna namna unaweza kuathiri hilo.
Hivyo kufanya au kutokufanya kitu kwa lengo la kuwaridhisha wengine, ni kujipoteza wewe mwenyewe.
Lengo lako kuu ni kuwa wewe halisi kwako na kupata kile ambacho una msukumo mkubwa wa ndani yako kukipata.
Mengine yote hayana umuhimu mkubwa kwako.
Amini zaidi maoni yako kuliko maoni ya wengine, kwa sababu hayo ndiyo yaliyobeba ukweli kuhusu wewe.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu hakuna kingine muhimu. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/09/3296
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kutokuangalia wengine wanavyokuchukulia bali kujiamini na kujikubali wewe mwenyewe na kufanya makubwa.
Kocha.
💯