💯KCM2324073; Kutokufanya.

Tumejipata, Tunaachilia Breki.

#JumatanoYaUwajibikaji

Mwanamafanikio,

Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.

Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.



💯 Neno la leo; Kutokufanya.

Leo ikiwa ni #JumatanoYaUwajibikaji tunaona jinsi ambavyo tunawajibika kwa makosa ya kutokufanya.

Kwenye maisha huwa kuna makosa ya aina mbili.
Moja ni makosa ya kufanya, yaani unafanya na unakosea.
Na mbili ni makosa ya kutokufanya, yaani unakuwa umekosea kwa sababu hujafanya.

Watu huwa wanaepuka kufanya ili wasikosee na kulaumiwa.
Wanadhani kwa kutokufanya basi hawatawajibika.
Lakini ukweli ni inapokuja kwenye maisha yako, unawajibika kwa kila kitu.
Kama hujapata unachotaka au hujafika unakotaka, ni wewe ndiye unayewajibika.
Iwe umefanya au hukufanya, unawajibika.

Kwa maana hiyo basi, ni bora makosa ya kufanya kuliko makosa ya kutokufanya.
Yaani kwa kuwa unawajibika kwa kila aina ya matokeo, ni bora ufanye na ukosee, kuliko kutokufanya na ukakosea.
Kwa sababu ukifanya na ukakosea unajifunza mengi, ya kufanya kwa usahihi zaidi wakati mwingine.
Wakati usipofanya na ukakosea, unakuwa hauna ulichojifunza.

Huwezi kukimbia uwajibikaji kwenye maisha yako.
Unaweza kutamani kuwalalamikia na kuwalaumu wengine, lakini ndani yako mwenyewe unajua ni wapi ulipozingua.
Usiache kufanya kwa kudhani hutawajibika.
Matokeo ya mwisho ndiyo yatakayokuwajibisha.
Hivyo hata ukikosea, kwa kuboresha zaidi utapata matokeo mazuri.

Kutokuwajibika ni breki inayowazuia wengi kupata mafanikio makubwa.
Achilia breki hiyo kwa kuwajibika kwa kila kitu kwenye maisha yako.
Wajibika kwa matokeo yoyote unayoyapata, iwe umefanya au hukufanya.
Unapowajibika, unashika hatamu ya kuyafanya mambo kuwa kwa namna unavyotaka wewe.

💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.

Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu uko sahihi kabisa. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/10/3297

Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuwajibika kwa kila kitu kwenye maisha yako, iwe umefanya au hujafanya.

Kocha.
💯