Kwenye maisha huwa kuna vitu ambavyo mtu huwa unakutana navyo na vinavuruga kabisa mpango uliokuwa nao awali. Hilo lilitokea kwangu tarehe 15/11/2011 pale niliposimamishwa masomo ya chuo kikuu kwa muda usiojulikana.
Kwa kipindi chote cha masomo yangu nilikuwa naishi kwenye hadithi ya ‘NENDA SHULE, SOMA KWA JUHUDI, FAULU VIZURI, UTAPATA KAZI NZURI NA KUWA NA MAISHA MAZURI.’ Hivyo nilisoma sana na nilifaulu sana, lakini ndiyo hivyo nikajikuta kwenye hali ya kuwa nje ya masomo kabla ya kuhitimu.
Kwa sababu kwa maisha yangu yote nimekuwa na kiu ya kuwa tajiri mkubwa na kupata mafanikio makubwa, nilianza kujiuliza nawezaje kupata mafanikio makubwa hata kama sina shahada. Nilitafuta sana mtandaoni na nikakutana na vitabu mbalimbali.
Ni utafutaji huo ndiyo ulinifikisha kwenye vitabu vitatu ambavyo ndiyo vimeyabadili kabisa maisha yangu. Vitabu hivyo ni RICH DAD POOR DAD, THE RICHEST MAN IN BABYLON na THINK AND GROW RICH.

Kitabu cha RICH DAD, POOR DAD kilinionyesha jinsi ambavyo elimu kubwa inaweza kuwa kikwazo kwa mtu kujenga utajiri. Mafunzo ya kitabu hicho yanawalinganisha baba wawili, mmoja mwenye elimu kubwa na ameajiriwa na mwingine mwenye alimu ndogo na anafanya biashara.
Kitabu hicho kilinifungua sana, kiasi cha kuona hakuna mtu anayeweza kushindwa kwenye maisha kwa sababu hana elimu kubwa. Badala yake kukosa elimu ndiyo kunaweza kuwa na manufaa zaidi. Japo nilirudi kumaliza masomo ya udaktari, kuhitimu na hata kufanya kazi miaka kadhaa kama daktari, masomo ya kitabu cha RICH DAD, POOR DAD yamekuwa nguzo kubwa sana kwangu kwenye kujenga biashara na kufanya uwekezaji.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha masomo ya msingi kabisa kutoka kwenye kitabu hicho cha RICH DAD, POOR DAD ambayo kila mtu mwenye kiu ya kujenga utajiri na mafanikio kwenye maisha yake anapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi.
Karibu ujifunze masomo hayo kwa kusikiliza kipindi hicho hapo chini.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.