Maisha yana changamoto nyingi sana. Na changamoto hizo hazitakoma kwa kipindi chote cha uhai wetu. Ukitatua changamoto moja, unakuwa umezalisha changamoto nyingine.

Wengi wamekuwa wanakata tamaa kwa mfululizo huo wa changamoto na kushindwa kuendelea na safari ya mafanikio. Hili huwatokea wengi pale wanapokuwa wameshafanikiwa sana wakiwa wametokea chini.

Hiyo ni kwa sababu mafanikio huwa yana tabia ya kuwasahaulisha watu kule walikotoka. Wakati mtu anaanzia chini, anakuwa anajituma sana kitu kinachompa mafanikio makubwa. Akishafanikiwa anaacha kupambana na kuanza kulinda.

Anapokutana na changamoto ambayo inaathiri mafanikio yake, anaona hawezi kuyajenga tena, hivyo anakata tamaa na kuanguka kabisa.

Falsafa ya Ustoa ni falsafa ya vitendo inayowawezesha watu kuishi maisha bora kwa kuzingatia asili ya binadamu. Kinachotutofautisha binadamu na wanyama wengine ni uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi.

Hivyo kama mtu utaweza kutumia akili yako kufikiri na kufanya maamuzi, utaweza kuvuka chochote unachokutana nacho kwenye maisha yako na kupiga hatua kubwa. Na hapo ndipo falsafa ya Ustoa inapokuwa na umuhimu kwenye maisha.

Kuna mazoezi kumi ya falsafa ya Ustoa ambayo mtu unapaswa kuyafanya kila siku ili uweze kuwa na maisha bora bila ya kujali unapitia nini. Moja ya mazoezi hayo linakuandaa pale unapopoteza vitu ulivyonavyo usiumie sana wala kukata tamaa. Yaani hata kama watu wa karibu sana kwako wamefariki, utaweza kulipokea hilo kwa utulivu na maisha yako yakaendelea.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha mazoezi hayo kumi na jinsi ya kuyafanya ili kuwa na maisha bora. Sikiliza kipindi hicho hapo chini na ukatumie mazoezi hayo kuvuka kila unachokabiliana nacho kwenye maisha yako.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.