Shughuli unazofanya za kuingiza kipato ni mbegu ya kujenga utajiri. Lakini kama ilivyo kwa mbegu yoyote ile, ili iweze kukua na kuzaa matunda, lazima ipandwe, kunyeshewa, kuwekewa mbolea na kupaliliwa.

Hivyo kuwa na kipato pekee haitoshi kujenga utajiri, unapaswa kukifanyia jambo la ziada ili kipato hicho kiweze kuwa na manufaa makubwa kwako.

Na hapo ndipo uwekezaji unapokuwa muhimu kwenye kujenga utajiri. Kwani ni kupitia uwekezaji ndiyo unaweza kutumia kipato kidogo unachokuwa nacho kujenga utajiri mkubwa.

Kwa bahati mbaya sana, uwekezaji ni kitu ambacho kimekuwa hakifundishwi wazi kwa watu. Siyo mashuleni wala majumbani. Hivyo wengi wanaingiza kipato na kutumia chote bila ya kufanya kabisa uwekezaji.

Wengi uwekezaji ambao huwa wanaufikiria ni kwenye mali, kama mashamba, viwanja na nyumba. Ni kweli hivyo ni uwekezaji, lakini siyo uwekezaji pekee ulipo. Na mara nyingi uwekezaji wa mali huwa unahitaji kiasi kikubwa cha fedha. Hilo hupelekea wengi kudharau fedha ndogo ndogo wanazopata na kuona haziwezi kuwekeza kwenye mali.

Huwa kuna kauli za utani ambapo watu wanaambiana fedha ndogo ndogo kama elfu moja haiwezi kujenga, hivyo watu wale na kunywa vile wanavyotaka. Lakini huo siyo ukweli, fedha hizo ndogo ndogo zina nguvu ya kujenga utajiri mkubwa pale mtu anapojua njia sahihi ya kufanya hivyo.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha sheria 10 za kujenga utajiri mkubwa kupitia uwekezaji mdogo mdogo. Hizi ni sheria ambazo mtu yeyote atakayezifanyia kazi ataweza kujenga utajiri mkubwa hata kama kipato chake ni kidogo.

Karibu usikilize kipindi hiki, uzijue sheria hizo 10 na kuanza kuzifanyia kazi mara moja ili uache kula mbegu za utajiri zinazopita kwenye mikono yako. Kipindi kiko hapo chini, karibu usikilize.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.