💯KCM2324089; Kuongeleana.
Tumejipata, Tunaachilia Breki.
#IjumaaYaMawasiliano
Mwanamafanikio,
Mwaka wa mafanikio 2023-2024 tumejipata kwa kuchagua kufanyia kazi kwa ukubwa kitu kimoja mpaka kitupe mafanikio makubwa tunayoyataka.
Tumeachilia breki kwa kufanyia kazi maeneo sita; MALENGO, KUJIKUBALI, UWAJIBIKAJI, UBUNIFU, MAWASILIANO na UTULIVU ili kujipa uhakika wa kufanya makubwa.

💯 Neno la leo; Kuongeleana.
Leo ikiwa ni #IjumaaYaMawasiliano tunaona jinsi ambavyo matatizo mengi duniani yanaweza kutatuliwa kwa watu kuongea badala ya kuongeleana.
Matatizo mengi duniani huwa yanatokana na hali ya watu kupenda kuongeleana badala ya kuongea.
Kuongeleana ni pale watu wanaposema mambo ya asiyekuwepo.
Huu ndiyo umbeya na majungu ambayo yamekuwepo na huzalisha matokeo yasiyo mazuri.
Kinachotakiwa kwenye maisha ni kuongea na watu moja kwa moja pale kunapokuwa na kitu kinachowahusu.
Badala ya kwenda kuwaongelea kwa watu wengine, ni vyema kuwakabili na kuongea nao.
Kuwaongelea watu huwa hakutatui chochote. Bali kunazidisha matatizo kuwa makubwa.
Kuwakabili watu na kuongea nao kuna nguvu ya kutatua mengi yanayokuwa yanaendelea.
Mawasiliano mazuri ni silaha muhimu kwenye kujenga na kuimarisha mahusiano baina ya watu.
Pale mahusiano yanapoanza kuzorota, tatizo linakuwa limeanzia kwenye mawasiliano.
Kama una jambo lolote kuhusu mtu, mkabili na ongea naye kuhusu kuhusu jambo hilo. Mtapata nafasi ya kulitatua na kusonga mbele.
Lakini kama utaenda kuongelea jambo hilo kwa wengine ambao hawahusiki, utazidi kukuza tatizo zaidi.
Ongea na watu badala ya kuwaongelea watu na utaweza kujenga mahusiano bora yanayoanzia kwenye hayo mawasiliano sahihi.
💯Hatua za kuchukua leo;
1. Andika ahadi yako ya mwaka wa mafanikio 2023-2024 kwa mtiririko wa NINI, LINI, WAPI, KWA NINI, NANI, VIPI na HISIA kisha weka kwenye kundi.
2. Soma kurasa 10 za kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO na shirikisha uliyojifunza kwenye kundi.
3. Chukua hatua kwenye yale ambayo umeshajifunza na shirikisha kwenye kundi.
4. Matokeo unayopata yashirikishe kwenye kundi.
5. Kaa kwenye mchakato sahihi wa kile unachotaka kufikia na epuka usumbufu unaokuwa kikwazo kwako.
Makala ya ukurasa wa leo ni kuhusu juhudi kutokuzaa matunda. Isome, weka maoni na nenda kachukue hatua. Fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2024/01/26/3313
Ukawe na siku bora kabisa ya leo, siku ya kuongea na watu badala ya kuwaongelea watu kwa wengine.
Kocha.
💯