3315; Ugumu wa kuanza.
Rafiki yangu mpendwa,
Kauli ya mwanzo ndiyo mgumu ni kauli ya kweli na yenye nguvu kwenye ufanyaji wa kitu chochote kile.
Kupanga huwa ni rahisi, kwamba nini unataka na utakipataje kwa kufanyaje, hilo wengi wanafanya.
Lakini inapofika wakati wa kuanza kufanya, wengi husogeza mbele kwa kuona bado hawajakamilika.
Zoezi hilo la kuahirisha kuanza huwa linaenda kwa muda mrefu mpaka kufikia mtu kutokufanya kabisa.
Kitu chochote kile huwa kinaonekana ni kigumu sana kabla ya kuanza kufanywa.
Hiyo ni kwa sababu mtazamo ambao watu wanakuwa nao siyo sahihi na wala hauendani na uhalisia.
Watu hudhani wanahitaji maandalizi makubwa sana ndiyo waweze kuanza kufanya.
Huona kutakuwa na vikwazo vingi kwenye ufanyaji hivyo kujipanga zaidi ili waweze kuvivuka.
Lakini ukweli ni kwamba kile watu wanachofikiria sivyo uhalisia ulivyo.
Ndiyo maana wengi wanaojisukuma na wakaanza kufanya huwa ni rahisi kwao kuendelea kufanya.
Hiyo ni kwa sababu uhalisia waliokutana nao unakuwa tofauti na mategemeo waliyokuwa nayo.
Ni muhimu sana ujenge tabia ya kuanza kufanya kila unachokuwa umepanga kufanya.
Hata kama unajiona hujawa tayari, wewe anza, itakuwa rahisi zaidi kwako kuendelea kufanya.
Japo kuna changamoto nyingine ya watu kuanza na kuishia njiani, angalau kuanza kunaleta alama ya tofauti.
Wajibu wako mkuu unapaswa kuwa ni kuanza kufanya, kisha kuendelea kufanya bila kuacha.
Jua kila kikwazo utakachokutana nacho kina jawabu na unaweza kuvuka na kuendelea.
Ugumu unaouona kabla ya kuanza kitu huwa ni tofauti kabisa na uhalisia wa baada ya kuanza kufanya.
Kinachoonekana kutokuwezekana kabisa kabla ya kuanza, kinawezekana baada ya kuanza.
Anza kufanya kila unachopanga, tena anza kufanya ukiwa na moto wa kupanga.
Usijali sana utaendeleaje, kwa sababu utalivuka daraja pale unapolifikia.
Anza na kabiliana na kila linalokuja mbele yako.
Hiyo ndiyo njia ya uhakika ya kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha. Hofu ya kuanza ni kikwazo kikubwa. Kwenye kupiga hatua. Ni muhimu kuanza mengine ya uboreshaji yatafuata baadaye.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike