Sisi binadamu tuna matakwa mbalimbali. Matakwa hayo ndiyo yanayotusukuma kwenye mambo yote tunayofanya. Tunawahi kuamka asubuhi na kuchelewa kulala tukiyahangaikia hayo tunayotaka.

Lakini pamoja na kutoa sehemu kubwa ya maisha yetu kuhangaika yale tunayotaka, bado ni watu wachache sana wanaopata kile hasa wanachotaka. Walio wengi huishi maisha ya kuhangaika lakini wasipate kile wanachotaka.

Tofauti ya wale wanaopata wanachotaka na wanaokosa haitokani na uwezo ambao watu wanao. Bali inatokana na namna watu wanavyoendea kile wanachotaka.

Namna ya ufanyaji ndiyo inawatofautisha wale wanaopata wanachotaka na wale wanaokosa. Wanaopata wanachotaka huwa wanafanya tofauti kabisa na wale ambao hawapati wanachotaka.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimekushirikisha kwa kina jinsi unavyopaswa kufanya ili uweze kupata chochote unachotaka. Kupitia kipindi hicho unajifunza kufanya kwa usahihi ili uweze kupata matokeo makubwa. Karibu uangalie kipindi hicho uweze kujifunza na kuchukua hatua sahihi ili upate kile hasa unachotaka.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.