Juhudi na mafanikio ni vitu viwili ambavyo watu wamekuwa wanashindwa kuvielewa vizuri. Hiyo ni kwa sababu wale wanaoonekana kuweka juhudi kubwa ndiyo huwa wana mafanikio kidogo, wakati wenye mafanikio makubwa hawaonekani kuweka juhudi kubwa.
Hilo limekuwa linawafanya wale ambao hawajafanikiwa wadhani kutakuwa na siri za ziada ambazo wale wanaofanikiwa wanazijua ila wao hawazijui. Kwa sababu wanashindwa kuelewa kwa nini licha ya juhudi kubwa wanazoweka bado hawafanikiwi.

Ni kweli wale wasiofanikiwa wanaweka juhudi kubwa sana, lakini bado hawafanikiwi. Sababu kubwa ni kwamba kuna vitu ambavyo vimekuwa vinakwamisha juhudi wanazoweka zisiwazalishie matunda.
Wanakuwa wanaweka juhudi kubwa sana, lakini pia wanakuwa na vizuizi vinavyofanya juhudi hizo zisiwazalishie matunda. Hilo ndiyo limekuwa linapelekea watu kufanya kazi au biashara kwa miaka mingi na bado hawapigi hatua kubwa kama wanavyotaka.
Kwa asili, kila kitu kina nguvu ya ukuaji ndani yake. Ndiyo maana mtoto mdogo akizaliwa, kinachofuata ni yeye kukua, hatua kwa hatua. Kama mtoto hakui kama alivyotegemewa, inajulikana kuna tatizo na hilo hutatuliwa ili akae sawa.
Kadhalika, mafanikio yanataka mtu aweke juhudi na pale juhudi zinapowekwa, zinatakiwa kuzalisha matokeo. Pale juhudi zinapowekwa lakini zisizalishe matokeo ni kwa sababu ya vizuizi ambavyo vinakuwepo.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimekushirikisha vikwazo vitatu ambavyo vimekuwa vinakwamisha juhudi kubwa unazoweka. Karibu uangalie kipindi hicho, ujifunze na kuviondoa vikwazo hivyo ili juhudi unazoweka ziweze kuzalisha matunda mazuri.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.