Watu wengi wamekuwa wanalalamikia huduma za mafunzo, ushauri na ukocha kama haziwi msaada kwao kutokana na kutokuona matokeo waliyokuwa wanayategemea.

Kitu kimoja ambacho watu hao wanakuwa hawakiangalii ni kwamba hakuna mafunzo, ushauri au ukocha utakaofanya kazi kwa mtu bila ya yeye mwenyewe kuufanyia kazi.

Watu wanaodhani mafunzo, ushauri na ukocha ni njia ya mkato ya kupata kile wanachotaka bila ya kuweka kazi, huwa wanapata tabu sana.

Kuna mambo mengi ambayo kila anayetaka kunufaika na huduma hizo za mafunzo ushauri na ukocha anapaswa kuyazingatia. Lakini kuna matatu ya msingi sana ambayo lazima mtu ayafanyie kazi ndiyo vitu hivyo viweze kufanya kazi kwake.

Haijalishi umeingia gharama kiasi gani kupata mafunzo na ushauri, kama hayo mambo matatu hutayazingatia, utabaki pale pale ulipo licha ya kupata maarifa na miongozo sahihi.

Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha mambo hayo matatu ya msingi unayopaswa kuyazingatia. Karibu ukiangalie kipindi, ujifunze na ukayazingatie haya ili mafunzo yote unayoyapata yakuwezeshe kufanya makubwa.

Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani,

Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi

0678 977 007 / amakirita@gmail.com

www.amkamtanzania.com

MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.