Kwenye kitabu cha The Alchemist, mhusika mkuu anasafiri kwenda eneo la mbali ili kuipata hazina yake. Inakuwa ni safari ya mateso, iliyojaa vikwazo vya kila aina. Na anapofika alipoambiwa hazina yake ipo, anagundua ni pale pale alipoanzia.
Kwenye maisha tumekuwa tunahangaika na siri nyingi za mafanikio, tukidhani kwamba kuna siri moja ya mafanikio ambayo tukiing’amua basi mafanikio yatakuwa rahisi kwetu. Lakini katika kukimbizana na hizo siri za mafanikio, watu wamekuwa wanaishia pale pale walipoanzia, wakiwa hawajapata walichotaka.

Ukweli kuhusu siri za mafanikio ni zipo, lakini ukweli mwingine wa kushangaza ni kwamba siri hizo hazijafichwa, bali zipo bayana kabisa. Kile kinachoitwa siri za mafanikio, ni vitu ambavyo vipo bayana kabisa. Vitu ambavyo mtu tayari anavijua, ila tu hajaweza kuvifanyia kazi na kunufaika navyo.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza dhana hii ya siri za mafanikio na jinsi ya kuweza kuzing’amua na kuzifanyia kazi ili mtu kupata mafanikio anayoyataka.
Karibu usikilize kipindi hicho hapo chini, jifunze na kuchukua hatua ili uweze kufikia mafanikio makubwa unayoyataka bila ya kukwamishwa na kitu chochote kile.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.