3333; Kila linalowezekana.
Kutoka mezani kwa Kocha,
Rafiki yangu mpendwa,
Katika kuonyesha kwamba mtu ameweka juhudi kubwa, huwa kuna kauli inayosema kila linalowezekana.
Mtu anasema amefanya kila linalowezekana, lakini bado hajapata matokeo aliyotarajia.
Ukweli ni kwamba, kama mtu amefanya kila linalowezekana, anastahili matokeo yoyote anayokuwa ameyapata.
Hiyo ni kwa sababu anachokuwa amefanya ni kidogo sana ukilinganisha na anachopaswa kufanya mpaka sasa.
Wengi hudhani kufanya kila linalowezekana ndiyo kiwango cha juu kabisa cha ufanyaji.
Hilo siyo kweli, kwa sababu linalowezekana ina tafsiri tofauti kwa watu tofauti.
Watu huwa wana mitazamo tofauti juu ya nini kinawezekana na nini hakiwezekani.
Wakati wale wanaofanikiwa wana mtazamo kwamba kila kitu kinawezekana, wanaoshindwa wana mtazamo kwamba vitu vingi haviwezekani.
Hivyo utayari wa kufanya makubwa kwenye makundi hayo mawili unatofautiana.
Kusema umafanya kila linalowezekana, wakati unaamini mengi hayawezekani, ni kiashiria tosha kwamba mengi hujayafanya.
Na hata ukiyafanya, ni rahisi kukata tamaa pale matokeo yanapokuja tofauti.
Kauli sahihi itakayokusukuma kufanya ni kufanya linalohitajika.
Hapa inakuwa tofauti kabisa, kwa sababu unafanya bila ya ukomo.
Hufanyi kwa sababu unaona inawezekana au haiwezekani, bali unafanya kwa sababu ndivyo inavyohitajika kufanyika.
Ili kupata matokeo makubwa, ya tofauti na yanayokupa mafanikio, ni lazima ufanye kwa tofauti kabisa na ulivyokuwa unafanya.
Kwa chochote unachofanya, nenda mbali zaidi kwenye ufanyaji.
Fanya kwa karidi ya inavyohitajika kufanyika na siyo kwa kadiri ya uwezo.
Wajibu wako mkubwa ni kufanya kwa namna ambayo matokeo yatakuja kwako bila ya shaka.
Hata kama yatachelewa, lakini kwa hakika yanakuja.
Na hilo litawezekana kama hakuna chochote kinachowazuia watu kwenye yale wanayoyafanya.
Usifanye kadiri ya uwezo wako, bali fanya kadiri ya inavyohitajika.
Wajibu wako mkuu ni kufanya ili kuzalisha matokeo makubwa, usikubali kukwamishwa na chochote.
Kwenye jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, ambayo ni jamii ya tofauti tunayoijenga, hatukubaliani na vikwazo vyovyote vinavyotuzuia kupata matokeo makubwa.
Mara zote tunachukua hatua kubwa na za tofauti ili kupata matokeo makubwa.
Ndani ya jamii ya KISIMA CHA MAARIFA, unafanya yote yanayopaswa kufanyika ili kupata matokeo makubwa.
Hujali wingi au ugumu wa yale yanayopaswa kufanyika, bali kinachoangaliwa ni matokeo yanayohitajika.
Ufanye utaratibu wa kwenda hatua ya ziada kwenye ufanyaji kuwa sehemu ya maisha yako na kwa hakika utaweza kufanya makubwa sana.
Ongozwa na matokeo na siyo uwezo, unaweza kudhani huna uwezo, lakini matokeo makubwa unayoyataka yatakufanya ufikie na kutumia uwezo mkubwa ulio ndani yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe